Usajili uliokamilika ligi kuu bara ‘Ligi Kuu ya Vodacom’ Simba, Yanga wamo

Mohamed Rashid, amefunga magoli 10 akiwa Tanzania Prisons ameonesha namna gani anajua kufunga ameungana na John Bocco na Emanuel Okwi wa Simba, ni usjaili...

Usajili uliokamilika ligi kuu bara ‘Ligi Kuu ya Vodacom’ Simba, Yanga wamo

Mohamed Rashid, amefunga magoli 10 akiwa Tanzania Prisons ameonesha namna gani anajua kufunga ameungana na John Bocco na Emanuel Okwi wa Simba, ni usjaili...

03 June 2018 Sunday 13:51
Usajili uliokamilika ligi kuu bara ‘Ligi Kuu ya Vodacom’ Simba, Yanga wamo

Na Amini Nyaungo

BAADA ya siku sita kupita tangu dirisha la usajili lifunguliwe, timu nne za ligi kuu Tanzania zimekamilisha usajili baadhi ya wachezaji.

Simba

Mabingwa wa ligi kuu bara tayari wameingiza wachezaji wa tatu wote walikuwa wafungaji bora katika timu zao.

Marcel Kaheza, amesajiliwa Simba akiwa mfungaji bora wa Majimaji na mfungaji namba tatu ligi kuu bara kwa magoli yake 14 msimu huu.

Mohamed Rashid, amefunga magoli 10 akiwa Tanzania Prisons ameonesha namna gani anajua kufunga ameungana na John Bocco na Emanuel Okwi wa Simba, ni usjaili uliokamilika pia.

Adam Salamba, ameonesha uwezo mkubwa sana imefika mahali Yanga nao walimtaka mwisho wa siku Simba wamepenyeza lupia ambayo alikuwa anahitaji ameanguka Simba, alifunga magoli 6 na ndiye mfungaji bora wa timu hiyo.

Yanga

Wameonekana kwenda mwendo wa kinyonga katika usajili lakini ndio wanavyokuwa wakati wote.

Marcelin Koukpo, raia wa Benin tayari ameanguka saini na klabu hiyo huenda leo akacheza katika michuano ya Sports Pesa Super Cup.

Azam

Azam nayo inataka watu wa kufanya kazi baada ya kocha Hans Van Pluijm sasa wamehamia katika usajili.

Donald Ngoma, tayari wamemtangaza kuwa mchezaji wao kwa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.

Tafadzwa Kutinyu naye amejiunga na Azam leo kuungana na Donald Ngoma na kocha wake Hans Van Pluijm

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Moodnass 2018-06-03 20:35:21

Hakika naiombea yanga yangu ipate boss tuweze kufanya usajili wa nguvu

Avatar
Kupililia 2018-07-26 21:59:29

Akika naiyombea yanga njaa izidi kushamili.

Avatar
MY NAME IS SELESTIN ,MWASHIUYA 2018-07-27 13:16:56

NAIOMBEA TEAM YANGU YA SIMBA IFANYE VIZURI KTK MICHUANO YAKIMATAIFA.208-209

Avatar
Side wa Arusha 2018-07-31 23:53:22

Naimbea timu yangu ya yanga maandalizi mema kambi popote siompaka uturuki kwani ligi itachezewa Tanzania wasiludi huko wakasingizia viwanja pasi hazipigiki.

Avatar
Naitwa Side wa Arusha. 2018-08-01 00:08:51

Mungu Ibariki yanga.

Avatar
MY NAME IS PACKSENCE 2018-08-02 16:55:31

Naitakia kheri timu yangu ya simba ktk msimu wa ligi kuu vodacom 2018-2019

Avatar
Naitwa yassin jafar wa CHAUWE TANDAHMBA 2018-08-04 09:40:12

Naitakia tm yangu ya simba maandaliz mema kwenye simba day.

Avatar
SAIMON RAPHAEL JIDALIMI 2018-08-11 12:06:41

poleni sana wanayanga jipeni moyo ipo siku nanyi mtatusua