banner68

Ustaa wa Salamba wateka mazoezi Simba

Mashabiki walalamikia juu ya uchezaji wake

Ustaa wa Salamba wateka mazoezi Simba

Mashabiki walalamikia juu ya uchezaji wake

11 July 2018 Wednesday 11:23
Ustaa wa Salamba wateka mazoezi Simba

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki wa Simba juzi walimvamia kaimu kocha mkuu wa timu hiyo Mrundi, Masoud Djuma na kuanza kulalamikia aina ya uchezaji wa mshambuliaji wake mpya, Adam Salamba.

Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi Jumatatu jioni mara baada ya mazoezi ya timu hiyo kumalizika Boko Beach Veterani jijini Dar es Salaam.

Salamba, alisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo hivi karibuni kwa dau la shilingi milioni 40, huku akipewa gari na nyumba ya kuishi aki­tokea Lipuli FC ya mkoani Iringa.

Kundi hilo la mashabiki walim­vaa kocha huyo na kumwambia anatakiwa kukaa kikao na msham­buliaji huyo na kumwam­bia aache kucheza kistaa kwani bado ana safari ndefu katika soka.

“Tunakuomba kocha ukae na Salamba na kumuonya kuwa yeye bado hajakuwa staa ndani ya Simba, ndiyo kwanza amesajiliwa hivi karibuni hana hata msimu mmoja.

“Katika michuano hii Kagame tumekuwa tukimfuatilia uwanjani akicheza kistaa kama ameshakuwa levo za akina Ronaldo (Cristiano) na Messi (Lionel) kitu ambacho siyo sawa, anatakiwa kubadilika na afahamu yeye bado.

“Kwa sababu ukimuacha aendelee kucheza kistaa mwisho wa siku ataigharimu timu kwa kupata matokeo mabaya, anatakiwa kucheza kwa kupambana kama alivyokuwa Rashid (Mohamed) na Marcel (Boniventure),” alisikika shabiki wa Simba huku kocha huyo akiitikia.

Kocha huyo al­imjibu shabiki huyo kwa kumwambia: “Hicho unach­okizungumza ni kweli kabisa, mimi nimeliona hilo na kulifanyia kazi na nilikaa naye kikao na kumuonya anatakiwa kubadilika na kuniahidi.

Championi

Keywords:
Masoud Djuma
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.