banner68
banner58

Utata wa Fei Toto kusaini klabu mbili tofauti, meneja atoa ufafanuzi

Utata wa Fei Toto kusaini klabu mbili tofauti, meneja atoa ufafanuzi

13 July 2018 Friday 09:09
Utata wa Fei Toto kusaini klabu mbili tofauti, meneja atoa ufafanuzi

Kukiwa na hali ya utata juu ya usajili wa mchezaji, kiungo Feisal Abdallah maarufu kama Fei Toto kusaini Yanga jioni ya jana huku saa kadhaa zilizokuwa zimepita akitambulishwa na Singida United, Meneja wake Mohammed Kombo, ametolea ufafanuzi juu ya suala hilo.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Kombo amesema mpaka kufikia saa 10 ya jana jioni Toto alikuwa mchezaji halali wa JKU na si Singida kama ambavyo vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo na mitandao blog hii vilivyokuwa vimeripoti.

Kombo ameeleza kuwa Singida hawakufanya naye mazungumzo yoyote na ameshangazwa na wao kumtangaza kama mchezaji wao bila kukamilisha taratibu rasmi ambazo zinapaswa kufuatwa ili kupata saini yake.

Meneja huyo amefunguka na kuwatupia lawama Singida kutangaza kuwa wameingia naye mkataba wa miaka mitatu wakati alikuwa ana mazungumzo na Yanga ambao walimuwahi na kufikia nao makubaliano.

Kutokana na sakata hilo, Yanga waliamua kuitisha kikao na Waandishi wa habari baada ya masaa kadhaa kupita wakimtabulisha kiungo huyo akitokea JKU na kuingia naye mkataba wa miaka miwili akiwa pamoja na Meneja wake, Kombo.

Baada ya tukio hilo kuibuka, baadaye Singida United kupitia Mkurugenzi wake, Festo Sanga alikuja kueleza kuwa Toto ni mali yao na tataribu zote rasmi za usajili walizifuata huku akisema utatuzi wa suala hilo wanaiachia TFF na Bodi ya Ligi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.