Uwanja wa Yanga Kigamboni bei mbaya

Uwanja wa Yanga Kigamboni bei mbaya

19 June 2019 Wednesday 09:25
Uwanja wa Yanga Kigamboni bei mbaya


Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
KLABU ya Yanga Africans imekabidhiwa rasmi kiwanja cha eka saba Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Eneo hilo lipo katika mtaa wa Kisarawe II, Kibada na thamani yake imetajwa kuwa ni takribani milioni 600 hadi 700.

Thamani hiyo imewekwa wazi na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Juni 18, 2019  alipokuwa akiwaonyesha  viongozi wa klabu ya Yanga eneo hilo.

Ijumaa ya Juni 20, 2019 Makonda anatarajia kuwakabidhi rasmi eneo hilo baada ya kukamilika kwa vibali vya umiliki

Juni 15, 2019 katika harambee ya kuchangia klabu ya Yanga iliyofanyika jijini Dar es Salaam , Makonda alitoa ahadi ya kutoa kiwanja hicho. 

Katika harambee hiyo takribani fedha milioni 700 zilitangazwa kupatikana  ikiwemo fedha keshi na ahadi.  

Updated: 19.06.2019 14:08
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
alan 2019-07-06 18:40:09

NDUGU zangu young

Avatar
alan 2019-07-06 18:40:36

NDUGU zangu young