banner68
banner58

Vilabu vinne Ligi Kuu England vyawania saini ya Mbwana Samatta

Everton inasemekana inaendelea kutafuta mshambuliaji wa kuziba pengo lililoachwa na Romelu Lukaku

Vilabu vinne Ligi Kuu England vyawania saini ya Mbwana Samatta

Everton inasemekana inaendelea kutafuta mshambuliaji wa kuziba pengo lililoachwa na Romelu Lukaku

09 October 2018 Tuesday 10:35
Vilabu vinne Ligi Kuu England vyawania saini ya Mbwana Samatta

Westham, Everton, Brighton na Burnley wanachuana kuipata saini ya nyota na nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta anacheza soka la kulipwa katika Ligi Kuu ya nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk.

Ripoti kutoka tovuti mbalimbali England zinaelezea namna gani timu hizo zinahitaji huduma ya mchezaji huyo ambaye amefanya vizuri akiwa Genk, moja ya tovuti maarufu kutoka katika mji wa Liverpool, Liverpool ECHO pamoja na mtandao wa HITC wamethibitisha uhitaji wa huduma ya Samatta ligi kuu England.

Mbwana Samatta tayari amefunga mabao kumi na nne katika michezo kumi na sita ya mashindano akiwa na Genk, nusu yake akiwa ni katika michuano ya Europa League.

Nyota huyo ameifungia timu yake ya Taifa ya Tanzania magoli 16 katika michezo 44 katika mashindano yote.

Thamani ya nyota huyo inafikia 4,00 Mill. € kwa viwango vilivyowekwa Septemba 11 mwaka huu

Samatta aliwahi kuwa mchezaji bora wa Afrika wakati anachezea TP Mazembe huku akiwa mfungaji bora msimu huo wa 2015.

Alitua KRC Genk mwaka 2016 akishuhudia wenzake wakipata nafasi ya kucheza ligi kubwa akiwemo Wilfred Ndidi aliyetimkia Leicester City huku wengine wakitua League 1 na Bundesliga.

Licha ya kutakiwa England bado Getafe ya Hispania inamfutilia kwa karibu nayo inahitaji huduma ya nyota huyo ambaye anafunga kila kukicha huko Ubelgiji.

Samatta ambaye ana miaka 25 inaonekana muda sahihi wayeye kucheza ligi kubwa na huenda akawa mchezaji wakwanza wa Tanzania kucheza ligi kuu ya England akiwa na vilabu vinavytofahamika.

Everton wanataka kuziba nafasi ya Lomelu Lukaku ambapo tangu aondoke bado pengo lake halijazibwa licha ya kusajili nyota kadhaa.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Zubeir mzuzuri 2018-10-09 14:15:38

Kila la kheri popa samagoals

Avatar
JONATHAN 2018-11-06 18:06:17

samatta anafaa kucheza ulaya.