Waamuzi wa Yanga dhidi ya Gor Mahia hadharani

Ni katika mashindano ya Kombe la Washindi barani Afrika

Waamuzi wa Yanga dhidi ya Gor Mahia hadharani

Ni katika mashindano ya Kombe la Washindi barani Afrika

13 June 2018 Wednesday 15:15
Waamuzi wa Yanga dhidi ya Gor Mahia hadharani

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi kutoka nchini Somalia kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi kati ya Gor Mahia ya Kenya na Young Africans ya Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Moi Kasarani Julai 18, 2018.

Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Hassan Mohamed Hagi akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Hamza Hagi Abdi, Mwamuzi msaidizi namba 2 Suleiman Bashir Abdi na Mwamuzi wa akiba Nur Muhidin Mohamed.

Mtathmini waamuzi anatokea Gabon Jan Olivier Mbera na Kamishna wa mchezo anatokea Africa Kusini Simphiwe Brian Xaba sambamba na mratibu wa mchezo huo Nomsa Jacobeth Mahlangu.

Aidha mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa July 29, 2018 Kwenye Uwanja wa Taifa wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Mauritius.

Mwamuzi wa katikati atakuwa Ahmed Imtehaz Heeralall akisaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Cauvelet Louis Ralph Fabian, mwamuzi msaidizi namba 2 Akhtar Nawaz Rossaye na Mwamuzi wa akiba Ganesh Chutooree.

Kamishna wa mchezo anatokea Zambia Patrick Kangwa, Mtathmini waamuzi anatokea Congo Louzaye Rene Daniel wakati Mratibu anatokea Nigeria Nasiru Sarkintudu Jibril.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.