banner68

Wanachama Yanga wamshukia Sanga suala la Tarimba

Wanachama Yanga wamshukia Sanga suala la Tarimba

12 July 2018 Thursday 10:41
Wanachama Yanga wamshukia Sanga suala la Tarimba

Baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga wameibuka kuzidi kutoa madukuduku yao kuhusiana na suala la Abbas Tarimba kuizulu kwenye Kamati ya Kuivusha Yanga wakati wa mpito.

Wanachama hao kutoka tawi la Tandale kwa Mtogole wameeleza kuwa kaimu Mwenyekiti wao, Clement Sanga amekuwa anaiendesha klabu kwa namna anavyotaka kuliko kuonesha kama yeye ni mtu wa mpira.

Mmoja wa wanachama kutoka tawi hilo amesema kuondoka kwa Tarimba ni kama pigo kwa Yanga kutokana na uweledi wake katika kazi kitu ambacho kimesababisha kila mtu kuibuka na maoni yake tofauti juu ya Sanga.

Aidha ameeleza kitendo cha kuivunja kamati kimyakimya si busara bila kukutana na Tarimba mwenyewe ambaye ni ndiye Mwenyekiti Mkuu.

Ikumbukwe Tarimba alipitishwa kushika wadhifa huo kupitia Mkutano Mkuu wa Yanga uliofanyika Juni 10 2018 katika ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam lakini hajamaliza hata miezi mwili ametangaza kujiuzulu.

Tarimba anakumbukwa na wanayanga kwa kuanzisha suala la Yanga kuwa kampuni kipindi akiwa kiongozi ndani ya klabu hiyo wakati huo kukiwa na kundi la Yanga asili waliokuwa wakipinga mchakato huo kutoka kwa Tarimba.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.