banner68
banner58

Wawa awakimbia Yanga atua Simba kwa mbwembwe

Wawa awakimbia Yanga atua Simba kwa mbwembwe

25 June 2018 Monday 08:47
Wawa awakimbia Yanga atua Simba kwa mbwembwe

Na Amini Nyaungo

Wakati dirisha la usajili likiwa bado lipo sehemu nzuri, mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Simba wamepindua meza kibabe kwa watani wao wa Jadi Yanga.

Hii imekuja  baada ya kumnyakua Serge Wawa ambaye alihusishwa kujiunga na wana Jangwani.

Wawa yupo nchini ambapo katika mazoezi ya Simba yaliyofanyika ‘weekend’ hii  walifanyia ufukweni ameonekana akiwa na jezi ya timu yake ya zamani ya Al-Merrikh akiwa katika mazoezi, pamoja na kocha wa Simba Masudi Djuma.

Yanga ilikuwa tayari imemalizana naye katika mazungunzo ya awali na imesemekana wamebakia kutuma tiketi ya  ndege ili aje amalizane kimaandishi, ila ndio hivyo kama ulivyosikia tena pesa ndio inaongea.

Wawa aliwahi kucheza Azam FC kwa mafanikio makubwa kwa misimu miwili 2014-2016 huku akiachwa baada ya  kupata mchongo wa kuelekea Al-Merrikh.

Simba inajiandaa na michuano ya Kagame itakayoanza wiki hii huku kukiwa na ongezeka la wachezaji  wapya watakao isaidia timu hiyo.

Updated: 25.06.2018 08:55
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.