banner68
banner58

Waziri Lugola: Kutekwa Mohamed Dewji, watu 20 wanashikiliwa

Waziri Lugola: Kutekwa Mohamed Dewji, watu 20 wanashikiliwa

13 October 2018 Saturday 19:49
Waziri Lugola: Kutekwa Mohamed Dewji, watu 20 wanashikiliwa

Serikali imesema imeshtushwa na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji 'MO' na kwamba mpaka sasa inashikilia watu 20.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo pamoja na matukio mengine kama hayo.

Lugola amesema matukio ya utekwaji yapo na jeshi la polisi lipo makini kuhakikisha wanadhibiti matukio hayo.

Amesema mpaka sasa bado nchi ipo salama na kwamba kufuatia kutekwa kwa MO wanawashikilia watu 20.

Aidha amesema ametoa maelekezo kwa jeshi la polisi kuhakikisha mtu yoyote anayeshikiliwa hakai ndani zaidi ya saa 24 endapo ataonekana hana hatia katika kiti anachochunguzwa.

"Tukio la kutekwa kwa MO kimetushtua sana na kwamba jeshi la polisi lipo makini na tunendelea kumtafuta na kuwatafuta wahalifu,"amesema Lugola.

Matukio yapo na jeshi la polisi tupo makini tunafuatilia na kuyadhibiti matukio yote kama haya.

"Tukio hili la MO tunawashikilia watu wasiopungua 20 tukitafuta taarifa tunazozitaka na siwezi kuwataja ni kina nani tunaowashikilia."

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.