banner68
banner58

Yajue ya kombe la Dunia 2018

Historia muhimu za kuelewa kuelekea Urusi

Yajue ya kombe la Dunia 2018

Historia muhimu za kuelewa kuelekea Urusi

28 April 2018 Saturday 16:57
Yajue ya kombe la Dunia 2018

Na Amini Nyaungo

Zikiwa zimebakia siku 47 kuelekea kombe la Dunia ambalo litafanyika nchini Urusi likishirikisha timu 32 kutoka mabara yote sita.

Kila timu inatarajiwa kuundwa hasa na wachezaji walioonyesha uwezo mkubwa katika ligi kubwa tano, hususani ile ya England ambayo imetoa zaidi ya wachezaji 30 katika mataifa yote.

Historia muhimu za kuelewa kuelekea Urusi

Brazil ndiyo timu iliyochukua mara nyingi kombe la dunia mara 5 kama miaka inavyosoma 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002 huku mwaka 1950 na 1998 alikuwa mshindi wa pili.

Germany imechukua mara nne mwaka 1954, 1974, 1990, 2014 huku ikiwa mshindi wa pili mara nne, 1966, 1982, 1986, 2002.

Italy pia haikuwa nyuma imenyakuwa mara nne 1934, 1938, 1982, 2006 akiwa mshindi wa pili mara mbili 1970 na 1994.

Argentina imenyakuwa mara mbili 1978 na 1986 na kuwa mshindi wa pili mara tatu 1930, 1990 na 2014.

Uruguay bingwa wa kwanza kuchukua kombe la Dunia amechukua mara mbili 1930 na 1950 haikuwahi kuwa mshindi wa pili.

France imechukua mara moja 1998 na kuwa mshindi wa pili mara moja mwaka 2006.

England hawa wazee wa vyombo vya habari wamechukua mara moja 1966 hawajawahi kuwa washindi wa pili.

Hispania licha ya kuwa nzuri imechukua mara moja tu mnamo mwaka 2010 haijawahi kuwa mshindi wa pili.

Uholanzi (Netherlands) haijawahi kuwa bingwa imecheza fainali nne 1974, 1978 na 2010.

Czechoslovakia hawa wajomba kabla hawajagawanyika kuwa mataifa ya Czech na Slovakia walipata kuingia fainali mara mbili 1934 na 1962.

Hungary nayo imeshiriki fainali mbili 1938 na 1954 kumbuka wakati huo ilikuwa mambo ni moto.

Sweden, taifa alilotoka Zlatan Ibrahimovic, wamefanikiwa kuingia fainali mara moja 1958 na kuambulia patupu.

Kwa takwimu hiyo ni miaka 88 hadi sasa tangu lianzishwe kombe hili.

Bado Brazil ndio mwamba akifuatiwa na Ujerumani na Italia kwa kuchukua mara nyingi, mfungaji bora wa muda wote kutoka Ujerumani ambaye ni Miloslav Klose akiwa amefunga jumla ya mabao 16 kwa kushiriki katika fainali nne za Kombe la Dunia.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Swedi anyitike 2018-06-11 21:57:47

Brazil nchiiliyo chukua Mara bingo Latino kwa