banner68
banner58

Yanga hawana tatizo na Ibrahim Ajib kurejea Simba

Yanga hawana tatizo na Ibrahim Ajib kurejea Simba

13 October 2018 Saturday 12:00
Yanga hawana tatizo na Ibrahim Ajib kurejea Simba

Siku chache tangu meneja wa mchezaji wa Yanga, Ibrahim Ajib kutamka kuwa kuna baadhi ya timu zimeonyesha kumhitaji mshambuliaji huyo, uongozi wa Klabu ya Yanga umeibuka na kusema hakuna kitu cha bure na yeyote anayemhitaji staa huyo aende mezani wakazungumze ikiwemo Simba.

Ajibu ambaye alisajiliwa na Yanga msimu uliopita akitokea Simba, amekuwa na kiwango bora msimu huu kwani mpaka sasa amehusika katika mabao nane na kutoa asisti sita huku akifunga mabao mawili.

Katibu wa Yanga, Omary Kaya alisema kuwa kiwango cha Ajibu kuongezeka ni jambo zuri na wao kama uongozi wanamuomba azidi kuongeza juhudi zaidi lakini hakuna taarifa ambayo ipo mezani kwake inayohusu timu kumtaka Ajibu hivyo kama wanamtaka waende kukaa mezani na siyo kuongea maneno pembeni kwani hakuna kitu cha bure.

“Taarifa hizo ndiyo kwanza nazisikia kwako wewe ila kwenye meza yangu hakuna barua ya timu ambayo inasema kuwa inamhitaji Ajibu lakini pia hakuna kitu cha burebure duniani, kwani hata ukimtaka mwanamke lazima umtongoze, hivyo kama wanamtaka Ajibu waje mezani tukae tuongee na siyo kuongea pembeni tu, wakija na pesa za kutosha sisi tunamuachia.

“Huwezi ukaanza ligi bila kujipanga, hivyo sisi kama uongozi wa Yanga tumejipanga kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri katika mechi zetu za ligi kuu na kurudisha heshima yetu,” alisema Kaaya.

Alipotafutwa Ajibu kuzungumzia ishu ya kutakiwa na timu kadhaa za Uarabuni, Afrika Kusini pamoja na Simba, simu yake iliita bila kupokelewa.

Updated: 13.10.2018 12:18
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Fofunatus Msita 2018-10-13 13:46:39

Busara itumike