Yanga kumpigia magoti Yusuph Manji

Mkutano huo wa viongozi wa matawi umefanyika kwa ajili ya kujiandaa na mkutano mkuu wa klanu hiyo utakaofanyika Juni 10 mwaka huu

Yanga kumpigia magoti Yusuph Manji

Mkutano huo wa viongozi wa matawi umefanyika kwa ajili ya kujiandaa na mkutano mkuu wa klanu hiyo utakaofanyika Juni 10 mwaka huu

07 June 2018 Thursday 13:58
Yanga kumpigia magoti Yusuph Manji

Na Mwandishi wetu

Wenyeviti wa matawi wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam wamekubaliana kwenda kwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji ili kumwomba kurejea na kuokoa hali ya mambo.

Katika mkutano wao uliofanyika jana, viongozi hao pia wamekubaliana kufanya mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa klabu hiyo kongwe nchini.

Mkutano huo wa viongozi wa matawi umefanyika kwa ajili ya kujiandaa na mkutano mkuu wa klanu hiyo utakaofanyika Juni 10 mwaka huu.

Kuelekea mkutano Mkuu wa Yanga utakaofanyika Juni 10, 2018, haya ndiyo maazimio ya mkutano wa matawi ya Yanga yaliyofanyika jana.

Miongoni mwa mambo mengine, pia viongozi hao walikubaliana kuhamasisha wanachama wa klabu hiyo kufika kwa wingi katika mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam siku chache zijazo.

Aidha, wadhamini wa klabu hiyo wakiongozwa na Mkuchika, Jaji Mkwawa, Francis Kifukwe na Mzee Jabir Katundu walikaa na Kaimu Mwenyekiti na kujadili Mkutano Mkuu na mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo ya mitaa ya Twiga na Jangwani.

Maazimio mengine, yaliyofikiwa kwenye kikao hicho ni kuipeleka klabu hiyo kwenye mabadiliko ili kuifanya klabu kuwa na uwezo wa kulipa mishahara ya wachezaji, kufanya usajili wa wachezaji wazuri na timu kuwa imara na yenye ushindani. Kamati ya mabadiliko inatarajia kutoa taarifa yake mbele ya wanachama wa Yanga siku ya Mkutano Mkuu.

Mkutano huo mkuu unatarajia kuhudhuriwa na Waziri Mwakyembe, Mkuchika na viongozi wote waandamizi wa serikali wadau wa Yanga.

Azania Post

Updated: 07.06.2018 15:41
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Erick chitumbi 2018-06-08 13:28:51

Ni wazo zuri na limekuja wakati mwafaka.mapito yaliyotukuta yanatosha na tusiwe wazoefu Kwenye magumu haya.tuamie Kwenye uelekeo wenye maslahi mapana ya club yetu.Mungu ibariki Yanga Afrika,Mungu ubariki mkutano mkuu wa juni10.