banner68
banner58

Yanga kuwafuata Gor Mahia Jumatatu Kombe la Shirikisho Afrika

Yanga kuwafuata Gor Mahia Jumatatu Kombe la Shirikisho Afrika

13 July 2018 Friday 12:07
Yanga kuwafuata Gor Mahia Jumatatu Kombe la Shirikisho Afrika

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini Julai 16 Jumatatu kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia, Julai 18 jijini Nairobi.

Yanga inashika mkia katika kundi lao kwa kuwa na pointi moja huku USM Alger ikiongoza kwa kuwa na pointi nne ikifuatiwa na Gor Mahia yenye pointi mbili na Rayon Sport ya Rwanda yenye pointi mbili pia.

Awali, Yanga ilikuwa iweke kambi ya siku chache Arusha kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo lakini imeshindikana na badala yake wanakwenda moja kwa moja.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Salehe amesema: “Maandalizi yanakwenda vizuri kama inavyotakiwa na wachezaji wote wameshaanza mazoezi kuelekea mchezo huo.

“Kwa sasa sijajua ni idadi ya wachezaji wangapi watakwenda huko lakini kwa upande wangu niliona ni vyema wachezaji wote wakaenda,” alisema Hafidhi.

Championi

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.