Yanga waomba kujitoa Kagame kuihofia Simba

Yanga waomba kujitoa Kagame kuihofia Simba

08 June 2018 Friday 11:22
Yanga waomba kujitoa Kagame kuihofia Simba

Na Amini Nyaungo

Umesikia habari za Yanga kombe la Kagame baada ya kupangiwa na Simba Julai 5 hapa Dar es Salaam, basi ndio hivyo tena wametuma barua wajitoe kuihofia Simba.

Yanga inaelezwa wametuma barua Shirikisho la Soka Tanzania TFF wajitoe katika michuano hiyo ili kujiandaa na michauno ya Shirikisho la Soka barani Afrika dhidi ya Gor Mahia.

Kutokana na muingiliano wa ratiba ya KAGAME na CAF, Yanga wameona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM Alger pia Rayon Sports ya Rwanda.

Baada ya taarifa hiyo inaonesha dhahiri Yanga wameikimbia Simba kama mashabiki wa timu hiyo wanavyodai hii kutokana na udhaifu wa kikosi hicho katika msimu wa ligi uliomalizika hivi karibuni.

Simba na Yanga zimepangwa pamoja kwenye kundi `C` ambapo kuna timu zingine ambazo ni Dakadaha ya Somalia pamoja na St. George kutoka Ethiopia.

Mashaindano hayo yanatarajia kuanza Juni 28 hadi Julai 13 ambapo mchezo wa Yanga na Gor Mahia utacheza Julai 15.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.