banner68
banner58

Yanga washtukia mchezo juu ya Ibrahim Ajib

Yanga washtukia mchezo juu ya Ibrahim Ajib

17 October 2018 Wednesday 14:27
Yanga washtukia mchezo juu ya Ibrahim Ajib

Dalili kwamba Simba imeanza kuvutiwa tena na kiungo wake wa zamani, Ibrahim Ajib, imewashitua Yanga.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, Uongozi wa Yanga umeanza kujifikiria kuhusiana na Ajib.

“Unajua Simba wameanza kuwapa Yanga presha kuhusiana na Ajib, maana ni kama wameanza kuvutiwa hivi.

“Uongozi wa Yanga unaliona hilo, tatizo hapa ni suala la fedha za kutosha lakini uongozi unaweza kujipanga.

“Tayari Ajib amekuwa mchezaji muhimu katika suala la kuiongoza timu maana asipofunga, atatengeneneza nafasi,” kilieleza chanzo.

“Juhudi zinafanyika kwa siri sana ili kuhakikisha fedha zinapatikana na Ajib anabaki Yanga.”

Hivi karibuni, Ajib amebadilika na kuwa moto wa kuotea mbali kwani pamoja na kutoa pasi murua za mabao amekuwa akifunga mabao yanayoacha gumzo.

Keywords:
Ibrahim Ajib
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.