banner68
banner58

Yanga watoa tamko juu ya Uchaguzi Mkuu

Yanga watoa tamko juu ya Uchaguzi Mkuu

01 November 2018 Thursday 10:48
Yanga watoa tamko juu ya Uchaguzi Mkuu

Wakati klabu ya Simba ikielekea kufanya uchaguzi wake mkuu Novemba 4, 2018, uongozi wa Yanga nao umetangaza kuweka hadharani mchakato wa uchaguzi wao leo.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu, Omar Kaya, ameeleza kuwa uongozi utaeleza kila kitu kuhusiana na uchaguzi utakaofanyika kama utakuwa ni Mkuu ama wa kujaza nafasi.

Kaya ameeleza hivyo kutokana na matamko tofauti tofauti ya klabu hiyo siku zilizopita kusema watafanya uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi ambazo zipo wazi baada ya viongozi kadhaa kujiuzulu.

Viongozi kadhaa akiwemo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, pia aliyekuwa Katibu Mkuu, Boniface Mkwasa, waliachia ngazi na nafasi zao zikiendelea kuwa wazi mpaka sasa.

Mbali na nyadhifa hizo zilizo wazi, Yanga pia ilitoa matamko ya kueleza nafasi ya Mwenyekiti wao Yusuf Manji, itaendelea kuwepo kufuatia mkutano mkuu wa mwisho uliofanyika Juni 6 2018 kuamua Manji aendelee kukalia kiti hicho.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Ndivata rajab 2018-11-04 06:01:23

Bora yawekwe wazi ili tupumue