banner68
banner58

Yanga watoa tamko zito juu ya Mohammed Banka

Ni baada ya TFF kumuengua kikosini

Yanga watoa tamko zito juu ya Mohammed Banka

Ni baada ya TFF kumuengua kikosini

01 November 2018 Thursday 10:52
Yanga watoa tamko zito juu ya Mohammed Banka

Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kueleza kuwa Mohammed Banka hana sifa za kuwa mchezaji wa Yanga, uongozi wa klabu hiyo umesema umeshangazwa na kauli hiyo juu ya kiungo huyo.

Kwa mujibu wa TFF kupitia Ofisa Habari wake, Clifford Ndimbo, alieleza kuwa Banka mpaka sasa ni mchezaji wa Mtibwa Sugar kutokana na Yanga kushindwa kukamilisha taratibu za usajili wake.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Banka kupitia Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya Kanda ya Tano Afrika (RADO) kutangaza kumfungia mchezaji huyo kwa muda wa miezi 14, kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya Bangi.

Licha ya maamuzi ya kifungo kutolewa na kauli hiyo, Ten amefunguka kwa kusema inashangaza shirikisho hilo kutamka maneno hayo akisema walifuata taratibu za usajili kwa mfumo mpya wa TFF FIFA CONNECT.

Ten amesema ukiingia katika mfumo huo mpya, unaonesha kuwa Banka ni mchezaji wa Yanga na akisema walizungumza na Mtibwa mapema kabla ya usajili kufanyika.

Aidha, Ten ameeleza watatoa maelezo zaidi wakishapokea barua rasmi ya kufungiwa kwa mchezaji wao ambaye waliamini alikuwa na ndoto za kufanya vema msimu huu akiwa na wachezaji wenzake ndani ya uwanja.

Mnamo Disemba 9, 2017 Mchezaji huyo akiwa Machakos nchini Kenya alichukuliwa vipimo vya mkojo ambavyo vilisafirishwa kwenda kwenye Maabara ya WADA iliyopo Doha, Qatar kwa uchunguzi zaidi na majibu kurudi yakiwa na tuhuma hizo zinazomkabili.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.