banner68
banner58

Yanga yabakiza Wanigeria wawili kikosini

Kocha Zahera atoa baraka kwa wachezaji watatu wa kimataifa kupewa mikataba

Yanga yabakiza Wanigeria wawili kikosini

Kocha Zahera atoa baraka kwa wachezaji watatu wa kimataifa kupewa mikataba

12 July 2018 Thursday 10:27
Yanga yabakiza Wanigeria wawili kikosini

Benchi la ufundi la Yanga limebakiza wachezaji watatu wa kimataifa na kama mambo yataenda poa watapewa mkataba na timu hiyo.

Wachezaji 16 kutoka nchi mbalimbali Congo, Nigeria, Cameroon na Ghana walitua kwa ajili ya majaribio kikosini hapo ambapo 13 wamefungashiwa virago vyao kutokana na viwango vyao kutokubalika na kocha, Mwinyi Zahera huku watatu wakibaki.

Hata hivyo, bado hawajapewa mikataba, lakini kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, amesema kuwa kama wanataka wachezaji basi wawape hao watatu mikataba.

Mbali na hao, uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa wachezaji wake wote waliokuwa hawana mikataba wamesharejea na kuanza mazoezi akiwemo Kelvin Yondani.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa hawajaanza mazoezi ni pamoja na Yondani, Juma Abdul, Juma Makapu, Beno Kakolanya, Hassan Kessy, Geofrey Mwashiuya na Andrew Vincent ‘Dante’ ambao taarifa zinasema kuwa wote walianza mazoezi jana.

“Mazoezi ya timu yanaendelea kama tulivyopanga, wachezaji wetu wote ambao walikuwa hawajaanza mazoezi tayari wameshaanza baada ya madai yao kukamilika akiwemo Yondani.

“Kuhusu wachezaji waliokuja kufanya majaribio, kocha ameshawachuja na kubakiza watatu kati ya 16, Wanaigeria wamebaki wawili na Mkongo mmoja,” alisema mtoa taarifa huyo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Ally 2018-07-12 19:00:34

Iwe kweli tu

Avatar
akraman 2018-11-04 00:29:48

waongo 2