Yanga yasogeza mbele 'siku ya mwananchi'

Yanga yasogeza mbele 'siku ya mwananchi'

11 July 2019 Thursday 22:05
Yanga yasogeza mbele 'siku ya mwananchi'

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

KLABU ya Yanga imesogeza mbele kilele cha siku ya Mwananchi ambalo ni tamasha maalum la kutambulisha kikosi kipya cha Yanga SC lililopangwa kufanyika Julai 27.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Africans, Dismass Ten amesema hayo leo Julai 11, 2019 katika mkutano wake na wanahabari makao makuu ya klabu, Jangwani mjini Dar es Salaam.
Ten amesema kwamba sababu za kusogezwa mbele kwa Siku ya Mwananchi ni kupisha mchezo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka 2020 Cameroon kati ya Tanzania na Kenya.
Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Harambee Stars Julai 27, 2019 katika mchezo wa kwanza raundi ya kwanza ya mchujo wa kuwania fainali za CHAN 2020, michuano inayoshusisha wachezaji wanaocheza ligi za  ndani  kabla ya timu hizo kurudiana Agosti 2 mjini Nairobi.

"Na kwa sababu hiyo, tarehe mpya ya kilele cha Siku ya Mwananchi itatangazwa upya, lakini tayari kikosi cha Yanga SC kipo kambini mjini Morogoro chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Msambia Noel Mwandila kikijiandaa na msimu mpya'' amesema . 

Tayari Yanga SC imeimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wapya 14 ambao ni kipa Metacha Boniphace Mnata kutoka Mbao FC ya Mwanza alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka Azam FC, mabeki Muharami Salum Issa ‘Marcelo’ kutoka Malindi ya kwao, Zanzibar, Ally Mtoni 'Sonso' kutoka Lipuli FC ya Iringa, Ally Ally kutoka KMC ya Kinondoni, viungo wa ulinzi, Abdulaziz Makame kutoka Mafunzo ya Zanzibar na Mapinduzi Balama kutoka Alliance FC ya Mwanza, 

Wengine saba wote wa kigeni ambao ni kipa Farouk Shikalo kutoka Bandari ya kwao, Kenya, Sadney Urikhob kutoka Namibia, Lamine Moro kutoka Ghana, Juma Balinya kutoka Uganda, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana wote wa Rwanda, Mustapha Seleman kutoka Burundi na Maybin Kalengo kutoka Zambia.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.