banner68
banner58

Yanga yatoa tahadhari kwa Mbao FC

Yanga yatoa tahadhari kwa Mbao FC

06 October 2018 Saturday 08:39
Yanga yatoa tahadhari kwa Mbao FC

Uongozi wa klabu ya Yanga umeitahadharisha Mbao FC kuwa hawajaja Dar es Salaam kucheza na SImba.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika, akiwataka Mbao kujipanga vilivyo kwani wamedhamiria kutoa maangamizi.

Nyika ameeleza kuwa Mbao wanajiamini wakijua kuwa wamekuja kucheza na Simba kitu ambacho haitakuwa rahisi kwao kupata matokeo.

Mwenyekiti huyo ambaye pia yupo kwenye kitengo cha Kamati ya Mashindano amefunguka hayo baada ya Mbao hivi karibuni kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao wa jadi Simba huko CCM Kirumba, Mwanza.

"Awamu hii wanaenda kucheza na Yanga na siyo Simba, hivyo wanapaswa kujipanga kwa maana tumedhamiria kuchukua alama tatu," alisema Nyika.

Yanga itakuwa inawaalika Mbao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kesho Jumapili, mechi ikianza majira ya saa moja za usiku.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Ally 2018-10-07 17:32:52

Bless