Yusuph Manji ‘agoma’ kurejea Yanga

Yusuph Manji ‘agoma’ kurejea Yanga

12 June 2018 Tuesday 12:46
Yusuph Manji ‘agoma’ kurejea Yanga

Na Amini Nyaungo

Baada ya kuiona filamu ya wana Yanga Jumapili ya Juni 10 ya kuhitaji Yusuph Manji arejee katika nafasi yake ya Uenyekiti, bado kiza kimetanda kuhusu kukubali kwa Mwenyekiti huyo kurejea katika nafasi hiyo.

Habari ambayo imepatikana na Azania Post zinasema hapo jana kulikuwa na kikao cha kuweza kumuomba arejee katika nafasi hiyo.

Kikao hicho hakikuweza kufanikiwa kwani hakuweza kukubali huku akisema wasubiri atafakari.

Habari za ndani zinasema mapenzi binafsi ya klabu hiyo ndio zinamfanya afikikirie mara mbili anachohitaji kuiona timu ikifanya vizuri, hata kama hatokuwa mwenyekiti bado atakuwa anaendelea kusaidia timu hiyo.

Habari nyingine zinasema tayari amemtangulia rafiki yake ambaye walikuwa wanafanya kazi wakati anaongoza timu hiyo Abdallah Bin Kleb kuwa katika kamati maalumu, inaonyesha wazi kuwa kuna msaada mkubwa ataufanya katika klabu hiyo hata kama hatorejea katika nafasi yake.

Msemaji mkuu wa Yanga, Dismas Ten ameiambia Azania Post kuwa kama kuna jambo lolote kuhusu Manji watasema ila hakuna kitu kinginge kilichoendelea ujumbe wake umefika kutoka kwa wanachama.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
RAMADHANI(TORRES) 2018-06-28 23:29:53

manji anamambo mengine sio mnavyomfikiria nyinyi mtasubiri sana miaka hii ya MO, MR SIMBA

Avatar
Deograthias Bundala 2018-08-03 22:05:01

Yusuf manj nnakuomba rudi kwenye yanga yako inaelekea kubaya