Yusuph Manji kuteremsha kipa kutoka TP Mazembe

Adhamiria kukisuka kikosi cha timu hiyo ya Jangwani kuanzia nafasi ya kipa

Yusuph Manji kuteremsha kipa kutoka TP Mazembe

Adhamiria kukisuka kikosi cha timu hiyo ya Jangwani kuanzia nafasi ya kipa

14 June 2018 Thursday 13:26
Yusuph Manji kuteremsha kipa kutoka TP Mazembe

Na Amini Nyaungo

Kumekucha huko Jangwani katika klabu ya Yanga hii inaonesha dhahiri kuwa tajiri wa timu hiyo Yusuph Manji amerudi baada ya kuonesha jeuri waziwazi kuhitaji saini ya kipa namba mbili kutoka TP Mazembe.

Yanga wako tayari kutumia pesa baada ya kusuasua kwa kipindi kizima cha msimu uliomalizika hivi karibuni, sasa wamehamia katika kutengeneza nguzo imara kuanzia golini huku wakionyesha kuhitaji kumchukua Vumi Ley Matampi ambaye ni kipa namba mbili wa TP Mazembe.

Matampi ambaye ana umri wa miaka 29 amegoma kusaini mkataba mpya na timu hiyo akitaka kuwa golikipa namba moja huku kocha wa timu ya Yanga Mwinyi Zahera ametumia fursa hiyo kumshawishi huenda akitua bongo atakuja naye.

Iwapo watashindwa kumshawishi kipa huyo wa TP Mazembe kujiunga nao, Yanga wanampango wa kumrejesha kipa wao wa zamani Deogratius Munishi ‘Dida,’ ambaye anachezea timu ya Chuo Kikuu kimoja nchini Afrika Kusini ili kuanza kuonekana wakati wa michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika nafasi ambazo pia Yanga zimewaharibia msimu huu ni sehemu ya goli kipa ambapo Youthe Rostand alikuwa anafanya makosa sana.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.