banner68
banner58

Yusuph Manji mbioni kurejea Yanga?

Leo kuishuhudia timu yake ya zamani ikichuana na Waarabu Uwanja wa Taifa

Yusuph Manji mbioni kurejea Yanga?

Leo kuishuhudia timu yake ya zamani ikichuana na Waarabu Uwanja wa Taifa

18 August 2018 Saturday 06:14
Yusuph Manji mbioni kurejea Yanga?

Uongozi wa Yanga umemtangaza Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya USM Alger utakaopigwa Uwanja wa Taifa Jumapili hii.

Yanga itashuka dimbani kucheza mchezo huo wa mkondo wa pili baada ya kupoteza ule wa kwanza huko Algiers, Algeria kwa kufungwa mabao 4-0.

Mbali na Jenerali Mabeyo, uongozi wa Yanga umesema aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mfanyabiashara Yusuph Manji, naye atakuwepo Uwanjani hapo kuishuhudia timu yake.

Manji atakuwa anarejea rasmi Uwanja wa Taifa kuitazama Yanga ikiwa ni takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu atangaze kujizulu wadhifa wake ndani ya klabu hiyo.

Uwepo wa Manji unaweza kuwa baraka na neema kwa wadau, wanachama, wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo ambayo imekuwa ikipitia kipindi kigumu hivi sasa.

Mechi hiyo itapigwa majira ya saa 1 za usiku kwa mujibu wa ratiba na itaoneshwa mubashara na kituo cha Azam TV.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
GIFT CHOTA 2018-08-23 12:56:13

MANJI NI MFALME WA YANGA ASILI, YANGA KAMPUNI NA YANGA SPORT CLUB

Avatar
D. Bundala 2018-08-22 13:28:31

Manji ikamate mikono miwili timu yako ya yanga

Avatar
Mwarabu mweus 2018-08-31 17:25:54

Manji ndio naniiiiiiiiiiiii!

Avatar
Edwin Daud Malole 2018-09-02 08:38:19

tunashukur sana wanayanga kurudi kwa manji yanga hawa madela wanachonga sana

Avatar
Musa maganga 2018-09-07 21:13:43

Manji anazungua tu

Avatar
ANAF FURAHA 2018-09-13 20:53:34

atakama mufanyaje hamuiwezi simba