Zidane kuondoka na Cristiano Ronaldo Real Madrid?

Zidane kuondoka na Cristiano Ronaldo Real Madrid?

31 May 2018 Thursday 16:15
Zidane kuondoka na Cristiano Ronaldo Real Madrid?

Na Amini Nyaungo

Swali gumu la kujiuliza kocha gani atachukua mikoba ya Zinedine Zidane ambaye leo hii amefikia tamati ya safari yake ya miaka miwili na nusu ndani ya mabingwa hao wa Ulaya baada ya kutangaza kujiuzulu mchana huu.

Kufuatia kuondoka kwa Zidane huenda mastaa kibao wakaondoka akiwemo Cristiano Ronaldo ambaye matamshi yake muda mfupi. Huku Chelsea ambayo wengi wanaamini inapanga kuachana na kocha wao Conte na kuajiri kocha mwinginge, na huenda kocha huyo akawa ni Zinedine Zidane.

Lakini wapo wachambuzi wanaodai kwamba, kuondoka kwa Zidane basi kutamfanya mshambuliaji wake wa Kiingereza Gareth Bale kuendelea kubaki klabuni hapo baada ya kunukuliwa akisema hivi karibuni kwamba, ataondoka kwa kukosa kupangwa katika mechi nyingi muhimu.

Zidane ambaye amewahi kushinda vikombe kadhaa vikubwa barani Ulaya na ulimwenguni wakati wa uchezaji wake, sasa amefanikiwa kuiongoza kuongoza timu ya Real Madrid kushinda vikombe vitatu vya ligi mabingwa Ulaya mara tatu mfululizo, kitu ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya timu hiyo.

Zidane ametumia miaka 2 na nusu kuchukua UEFA Champions League mara 3 mfululizo rekodi ambayo itachukua miaka mingi kabla haijafikiwa na kocha na klabu nyingine, amechukua super cup mara mbili na klabu bingwa dunia kwa vilabu mara 2.

Kwa rekodi aliyoiweka kwa miaka miwili na nusu ameweza kuwazidi kina Arsene Wenger na Sir Alex Ferguson ambao wametumia miaka zaidi ya 20 kupata makombe mengi.

Ila rekodi hii haiondoi ubora wa Ferguson kuwa bora duniani.

Zidane ambaye ni raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria amezaliwa 23 Juni 1972 huko Marseille, France, amechukua kombe la dunia mwaka 1998 akiwa kama mchezaji, amechukua UEFA akiwa kama mchezaji amekuja kuchukua UEFA tena akiwa kama kocha mkuu.

Wapi ataelekea?

Baada ya kutangaza kuachia ngazi huenda kocha huyo ndiye anayetarajiwa kuja kuchukua mikoba ya Didier Deschamps ambaye anafundisha timu ya taifa ya Ufaransa.

Kwa kipindi hiki ambacho bado timu kama Chelsea wanahaha kumpata kocha mpya huenda siku zijazo zikaandikwa habari za kumuhusu kuelekea huko au hata Manchester United licha ya kumpa Mourinho mkataba mnono bado hawana furaha na kocha huyo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
salym khamis hamad 2018-06-26 17:00:27

0779109984