Iran yatoa masharti magumu kwa na wakaguzi wa nyuklia

IAEA ambayo inafuatilia utekelezaji wa masharti yaliyowekwa dhidi ya mipango ya nuklia ya Iran chini ya mkataba huo, inasema Iran inatekeleza ahadi zake...

Iran yatoa masharti magumu kwa na wakaguzi wa nyuklia

IAEA ambayo inafuatilia utekelezaji wa masharti yaliyowekwa dhidi ya mipango ya nuklia ya Iran chini ya mkataba huo, inasema Iran inatekeleza ahadi zake...

07 June 2018 Thursday 09:35
Iran yatoa masharti magumu  kwa na wakaguzi wa nyuklia

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Iran imesema haitaitikia wito wa kuitaka ishirikiane kikamilifu zaidi na wakaguzi wa nyuklia wa Umoja wa Mataifa hadi pale mkwamo kuhusu mustakabali wa makubaliano yake na mataifa yenye nguvu duniani utakapotatuliwa.

Balozi wa Iran katika Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki - IAEA Reza Najafi anasema wakati nchi hiyo haifadiki na mkataba huo, hakuna anayestahili kutarajia Iran kuzitekeleza zaidi hatua za hiari.

IAEA ambayo inafuatilia utekelezaji wa masharti yaliyowekwa dhidi ya mipango ya nuklia ya Iran chini ya mkataba huo, inasema Iran inatekeleza ahadi zake, lakini pia ikatoa wito wa ushirikiano wa haraka kuhusu utoaji ruhusa ya kufanya ukaguzi wa mapema.

Kiongozi wa IAEA Yukiya Amano alisema kauli yake sio ya kuelezea wasiwasi wala malalamiko bali ni ya kuihimiza Iran. Mataifa yenye nguvu ya Ulaya yanajitahidi kuuokoa mkataba huo tangu Rais Donald Trump alipoiondoa Marekani mwezi uliopita na kusema kuwa ataiwekea upya Iran vikwazo vikali zaidi.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.