Marekani, Iran zatambiana

"Hatua hii ni kutokana na kile alichodai kuwa ''tabia za uchokozi'' zinazodaiwa kufanywa na vikosi vya Iran.

Marekani, Iran zatambiana

"Hatua hii ni kutokana na kile alichodai kuwa ''tabia za uchokozi'' zinazodaiwa kufanywa na vikosi vya Iran.

18 June 2019 Tuesday 08:42
Marekani, Iran zatambiana

Tehran,Iran
WAKATI kukiwa na hali ya mvutano na Iran, Marekani inatarajia kutuma kikosi maalum cha wanajeshi zaidi ya 1000 kwenda Mashariki ya Kati

Waziri wa ulinzi  wa Marekani, Patrick Shanahan Jumatatu Juni 17, 2019 amesema hatua hiyo ni kutokana na kile alichodai kuwa ''tabia za uchokozi'' zinazodaiwa kufanywa na vikosi vya Iran.

Vikosi vya maji vya Marekani vimeonyesha picha mpya, wakiihusisha Iran na vitendo vya mashambulizi dhidi ya meli ya kubeba mafuta katika Ghuba ya Oman.

Iran ilitangaza siku ya Jumatatu kuwa haitatekeleza sehemu ya makubaliano ya mwaka 2015 kuhusu nyukilia.

Ilisema itavunja makubaliano yaliyofikiwa na mataifa yenye nguvu kuhusu zana za nyukilia ifikapo Juni 27, 2019.

Katika taarifa yake Shanahan amesema ''Marekani haitafuti mgogoro na Iran'' lakini hatua imechukuliwa ili ''kuhakikisha kunakuwa na usalama na ustawi wa wanajeshi wanaofanya kazi katika ukanda huo kulinda maslahi ya taifa''.

''Mashambulizi ya hivi karibuni ya Iran yanaonyesha wazi ni vitendo vya kichokozi vya vikosi vya Iran na mawakala wake ambayo yametishia wanajeshi wa Marekani na maslahi yake katika ukanda mzima.''

Amesema Jeshi litaendelea kufuatilia hali ilivyo eneo hilo na kufanya marekebisho ya vikosi ipasavyo.

Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu eneo gani Marekani itapeleka vikosi vyake.

Tangazo la Jumatatu kuhusu kuongezwa kwa idadi ya vikosi limekuja ikiwa ni kando ya lile la vikosi 1,500 vilivyotangazwa na Rais Donald Trump mwezi uliopita.

Waziri wa mambo ya nje, Mike Pompeo alisema siku ya Jumapili kuwa Marekani haikutaka vita na Iran, lakini hata hivyo ''imekuwa ikifikiria  namna ya kufanya''.
Kwa nini mvutano huu mpya?
Mwaka 2015, Iran ilikubali kutekeleza makubaliano yaliyowekwa na mataifa yenye nguvu kupambana na urutubishaji wa nyukilia.

ilikubali kiasi cha urutubishaji wa madini ya urani, ambayo hutumika kutengeneza silaha za nyukilia, na hatua nyingine ili kupata nafuu ya vikwazo.

Lakini Trump aliamua kuachana na mkataba huo mwaka 2018 na kuiwekea tena vikwazo.

Uamuzi huo uliathiri uchumi wa Iran, ambao ulitegemea sana mafuta, na Iran ikajibu kwa kuvunja makubaliano kuhusu nyukilia.

Siku ya Jumatatu, msemaji wa shirika lake la nguvu za Atomiki alisema Iran ina mpango wa kuvuka ukomo uliowekwa kuhusu urutubishaji madini ya urani katika kipindi cha siku kumi.

Lakini,Iran imesema bado ''muda upo'' kwa mataifa ya Ulaya kuchukua hatua kuilinda Iran dhidi ya vikwazo vya Marekani.

Marekani ilijibu kwa kushutumu Iran kwa kutumia nguvu kuhusu suala la nyukilia.

Uingereza, Ufaransa,Ujerumani zimeionya Iran kutokiuka mkataba wa mwaka 2015.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.