Marekani, Iran zazua taharuki eneo la Ghuba

Marekani, Iran zazua taharuki eneo la Ghuba

18 May 2019 Saturday 11:19
Marekani, Iran zazua taharuki eneo la Ghuba


Na mwandishi wetu, Mashiriki ya kati
Wakati hali ya taharuki ya vita kati ya nchi za Marekani na Iran, katika nchi za Ghuba Naibu Mkuu wa Majeshi ya Mapinduzi ya Iran amesema Makombora waliyonayo yana uwezo wa kuziangamiza manowari za kivita za Marekani zinazosonga kuelekea ghuba tayari kwa vita.


Mwanzoni mwa mwezi Mei 2019 Mshauri wa Taifa wa Mambo ya usalama wa Marekani,  John Bolton alitangaza  kutumika kwa manowari USS Abraham Lincon kwa ndege aina ya B 52 zitakazofanya mashambulizi dhidi ya Iran.


Baadae Wizara ya Ulinzi ya Marekani ikapeleka mabomu ya Patriotic ili kuweza kulinda manowari  hiyo isishambuliwe na mambo ya Iran.


Kiongozi huyo wa Iran amesema kuwa licha ya vitendo vyote vinavyotishia kuanza kwa vita baina ya Marekani na Iran kwa kile kinachodaiwa kinafanywa Marekani baada ya kubainika na ripoti za siri za kijasusi za Marekani, Iran imebaki kimya ikiendelea na shughuli zake bila kujibu vitisho hivyo.


Hata mambomu yetu ya masafa ya Kati yana uwezo mkubwa wa kufikia Manowari za marekani zilizopo Ghuba alisema Mohamed Saleh Jokar. Iran inaishambulia Marekani kuanzisha vita vya kisaikolojia dhidi ya Iran kwa kuanza kukusanya nguvu za kijeshi kwenye eneo la ghuba Hatua iliyofanya Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Javad Zarif kusema Iran haipo tayari kwa mazungumzo na Marekani


Wakati mvutano huo ukiendelea huko nchini Kuwait Kiongozi Mkuu wa nchi hiyo Emir Sheikh Sabah al Ahmed al Sabah ameyataka majeshi ya nchi yake kukaa katika hali ya tahadhari kutokana na Mvutano uliopo kati ya nchi za Marekani  na Iran ambao unatishia usalama wa eneo la ghuba.


Sheikh Sabah ametoa wito huo wakati akikagua majeshi ya taifa ya nchi hiyo na kunukuliwa na shirika la habari la Kuwait ( KUNA ) kuwa majeshi yake lazima yawe tayari kukabaliana na athari yeyote itakayotokea kuhusiana na vita hivyo.


Wakati hayo yakiendelea huko Ghuba Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza  Marekani haina nia yeyote ya kuishambulia Iran japo kuna taharuki hiyo hivi sasa

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.