Msikiti wa mwaka 1,200 wagunduliwa nchini Israel

Msikiti wa mwaka 1,200 wagunduliwa nchini Israel

19 July 2019 Friday 15:46
Msikiti wa mwaka 1,200 wagunduliwa nchini  Israel

Mojawapo ya misikiti ya kwanza iliyotambulika duniani, uliojengwa takriban miaka 1,200 iliyopita, umegunduliwa na wanaikiolojia katika jangwa la Negev nchini Israel.

Masalio hayo, ya kutoka karne ya 7 au ya 8 yaligunduliwa katika mji wa Bedouin - Rahat.  Ni msikiti wa kwanza unaotambulika katika eneo hilo kutoka wakati huo, ukishindana kwa umri na ule uliogunduliwa Makka na Jerusalem, IAA limesema.

Watafiti Jon Seligman na Shahar Zur wanasema msikiti, wa kutoka karne ya 7 au 8 ni jambo adimu kuligundua kokote. Watafiti wanaamini huenda wakulima wa eneo hilo ndio waliokuwa waumini waliosali katika msikiti huo.

Jengo hilo lilikuwa la wazi, lenye umbo la mstatili na lilikuwa na "Mihrab" - au upembe anaosimama muongoza sala linaloelekea mji mtukufu wa Makka au Qibla.

Ni mojawapo ya misikiti ya kwanza baada yakuwasili kwa Uislamu katika inayojulikana hii leo kama Israel wakati waraabu walipolitawala jimbo la Byzantine mnamo mwaka 636, kwa mujibu wa Gideon Avni, mtaalamu wa historia ya kale ya uislamu.

"Ugunduzi wa kijiji na msikiti katika eneo hilo ni mchango muhimu katika uchunguzi wa historia ya nchi hiyo wakati wa kipindi hicho kigumu," amesema.

Waislamu wanaswali katika enoe hilo kulikogunduliwa masalio ya mskiti

"Huu ni ushahidi wa lengo la jengo hili na lilivyotumika miaka mia kadhaa iliyopita," amesema Seligman.

Yaser Alamor anaonyesha jiwe lililogunduliwa katika msikiti huo


BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.