Mahakama, TTCL wasaini mkataba bilioni 4.17

Mahakama, TTCL wasaini mkataba bilioni 4.17

29 July 2019 Monday 16:38
Mahakama, TTCL wasaini mkataba bilioni 4.17

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam. 
MAHAKAMA ya Tanzania umeingia mkataba na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa ajili ya kuunganishwa katika mkongo wa taifa wa mawasiliano.

Mkataba huo wa miaka miwili, wenye thamani ya  bilioni  4.17, unatekelezwa katika mahakama 157 zilizopo hapa  nchi .

Mkataba huo umesainiwa leo Julai 29, 2019, na Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Husein Kattanga, katika kituo cha mafunzo kilichipo  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kabla ya kusainiwa kwa mkataba huo,  Mkurugenzi wa Tehama Mahakama ya Tanzania, Kalege Enock , alisema kuwepo kwa mtandao  wa intaneti kutasaidia  kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za Mahakama, mfano; shahidi anaweza kuwasilisha ushahidi bila kulazimika kufika Mahakamani, Wakili au Mwananchi anaweza kufungua shitaka au shauri kwa njia ya mtandao.

"  Mkataba huu ni unalenga kupanua matumizi ya TEHAMA katika ngazi zote za Mahakama ili kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati lakini pia kusogeza huduma za Mahakama karibu zaidi na wananchi" Alisema Enock na kuongez

" Mahakama imeingia mkataba na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa ajili ya kuunganisha majengo ya Mahakama katika mkongo wa mawasiliano wa taifa,  kuanzia Mahakama ya Rufani hadi Mahakama za Mwanzo zenye majengo ya kisasa" alisema Enock

Enock alizitaja mahakama ambazo zitaunganishiwa katika mkongo huo wa mawasiliano kuwa ni Mahakama ya Rufani moja,  Mahakama Kuu 16,  Mahakama Kuu Maalumu (Specialized Divisions) nne, Mahakama za Mkoa 29 ,  Mahakama 122 za Wilaya na  Mahakama 10 za  mwanzo ambazo kwa ujumla zitakuwa 157" alisema Enock.

Alisema huduma zitakazotokewa katika majengo hayo ni intaneti na data na kwamba Teknolojia hizo mbili zitatumika kutokana na mazingira ya kijiografia.

Enock alisema moja ya malengo katika mradi huu ni kuongeza ufanisi katika mtiririko mzima wa shughuli za Mahakama na kwa kuzingatia unyeti na usalama wa shughuli za Mahakama huduma hiyo ya mtandao itawezeshwa na teknolojia ya “Virtual Private Network (VPN)” kupitia ‘‘Multiprotocol Labelling Switch (MPLS).

Alisema kuwepo kwa mtandao kutawezesha wananchi kupata huduma kwa urahisi kupitia mifumo ya kieletroni ya Mahakama wakati wote na kutoka mahali popote walipo.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mahakama  Tanzania, Hussein Kattanga alisema Mahakama ya Tanzania inatekeleza mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia Julai 2015 hadi Juni 2020.

Kattanga alisema lengo kubwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za Mahakama kwa kupitia Mifumo ya kielektroni lakini pia kuweka  mazingira wezeshi ya kubadilishana taarifa kati ya Mahakama, taasisi  na wadau katika Mfumo mzima wa utoaji haki nchini.

" Huduma hii itarahisisha upatikanaji wa taarifa mbali mbali hasa mwenendo wa mashauri na shughuli za Mahakama kwa wananchi na wadau wengine kwa ujumla" alisema 

Naye, Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema watahakikisha kuwa wanatoa huduma bora.

" Mahakama ya Tanzania imefanya uamuzi sahihi kutuchagua sisi kuwahudumia, niseme tu tutakuwa sehemu ya kusaidia upatikanaji wa haki  kwa haraka , hivyo na sisi tunajiona ni sehemu ya mahakama" alisema Kindamba.

Updated: 29.07.2019 16:42
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.