Omar Nundu mwenyekiti mpya bodi ya Airtel Tanzania

Omar Nundu mwenyekiti mpya bodi ya Airtel Tanzania

12 June 2019 Wednesday 11:57
Omar Nundu mwenyekiti mpya bodi ya Airtel Tanzania

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
RAIS John Magufuli amemteua Mohamed Abdalallah Mtonga kuwa mwenyekiti wa  bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL)

Amechukua nafasi ya Dk Omari Nundu ambaye ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.

Uteuzi wa Nundu unafuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali na kampuni ya Bharti Airtel International juu ya uendeshaji wa Airtel Tanzania na kwamba mwenyekiti wa bodi atateuliwa na serikali.

Pia  Dk Prosper Godfrey Mafole ameteuliwa kuwa afisa mkuu wa ufundi wa Airtel Tanzania.

Wajumbe watakaoiwakilisha serikali katika bodi hiyo ni John Marato Sausi na Lekinyi Ngariapusi Mollel.

Uteuzi huo umenza rasmi leo Juni 12, 2019

Updated: 12.06.2019 12:05
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.