banner68
banner58

Bashe, Nape, Zitto, Polepole wajadili kuondoka Mtatiro CUF

Bashe, Nape, Zitto, Polepole wajadili kuondoka Mtatiro CUF

11 August 2018 Saturday 15:08
Bashe, Nape, Zitto, Polepole wajadili kuondoka Mtatiro CUF

Wanasiasa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini wametoa maoni tofauti kuhusu uamuzi wa mwanasiasa Julius Mtatiro aliyetangaza kuhama CUF na kuonyesha nia ya kuhamia CCM.

Mtatiro ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, amewaambia wanahabari leo Agosti 11, 2018 jijini Dar es Salaam kwamba, amejiuzulu CUF na yuko tayari kujiunga na CCM kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Magufuli.

Saa chache baada ya kutangaza uamuzi huo, wanasiasa mbalimbali waliibuka na kuandika kwenye mitandao ya kijamii wengine wakimpongeza na wengine wakimkosoa.

Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe ameandika kwenye ukurasa wake wa Twita ameandika akisema:

“Huko wanakokutegea kukufukuza kila usemapo ukweli? Ninaamini kwenye maendeleo ndani ya Demokrasia na siyo maendeleo ndani ya udikteta. Ninaamini katika uhuru wa fikra na siyo mawazo ya kiimla.Ninaamini nchi yetu inahitaaji chama kingine kuirudisha kwenye reli. Nafasi ya CCM ni Museum (makumbusho).

Mbunge wa Nzega, (CCM) Hussein Bashe ameujibu ujumbe wa Zitto akisema:

 “Ni rahisi kuleta mabadiliko ya haki, demokrasia na maendeleo ndani ya CCM) kuliko kutafuta mabadiliko nje kwa sababu kuna mgogoro wa kimawazo, kimuundo na kimadili huko nje. Kuna wanajeshi wachache wa ukweli.”

Kwa upande wake, Nape Nnauye Mbunge wa Mtama (CCM) ameandika akisema:

 “Tunachagua rangi ya Paka wakati shida yetu ni kukamata Panya.Nguvu tunayopoteza kuhoji rangi ya paka ingetumika kushughulika na panya tungekuwa mbali sana,”

Nape katika nukuu yake nyingine ameandika akisema:  

“Kama msomi wa Sayansi ya Siasa, naona hii ni fursa muhimu ya kujengwa kwa aina mpya ya vyama na siasa za upinzani nchini. Kwa demokrasia, hamahama hii muhimu itumike kama fursa ya kujenga upya uimara wa CCM unaotegemea ubora wa upinzani(Simba/Yanga).

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole yeye ameandika:

“Huu unaitwa uhuru wa kisiasa kwa mujibu wa katiba yetu, halafu wale wa ‘siasa za bei nafuu mseme kanunuliwa;” Hongera kaka, ndugu, kamaradi. Historia na Mungu pekee atakupa tuzo ya dhamira yako njema. Na mimi nimeikuta mtandaoni.”

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.