Bungeni leo: Wabunge CHADEMA wacharuka kubambikiwa kesi

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuph Masauni, alisema kuwa Mbunge huyo amekuwa akitoa madai hayo mara kwa mara bila uthibitisho...

Bungeni leo: Wabunge CHADEMA wacharuka kubambikiwa kesi

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuph Masauni, alisema kuwa Mbunge huyo amekuwa akitoa madai hayo mara kwa mara bila uthibitisho...

05 June 2018 Tuesday 12:11
Bungeni leo: Wabunge CHADEMA wacharuka kubambikiwa kesi

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Iringa mjini , Peter Msigwa (chadema) amemtuhumu Mkuu wa upelelezi mkoa hup (RCO) kwa kuwalazimisha wanachadema kujiunga na chama cha Mapinduzi, vinginevyo wanabambikiwa kesi.

Alikuwa akiuliza swali la nyoongeza bungeni leo ambao alisema kuwa tabia hiyo ya kubambikiwa kesi ipo sana kwani hata yeye yamemkuta.

Msigwa alitaka serikali kama ipo tayari kuchunguza tuhuma hizo za mkuu wa upelelezi huyo kuwalazimisha ili wasifunguliwe kesi.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuph Masauni, alisema kuwa Mbunge huyo amekuwa akitoa madai hayo mara kwa mara bila uthibitisho.

Alisema kuwa endapo ataleta ushahidi wa madai yake serikali haitasita kulifanyia kazi suala hilo mara moja.

Hata hivyo alibainisha kuwa hadi sasa hakuna askari ambaye amefanya vitendo hivyo ambavyo ni kinyume cha sheria.

Aliwataka wote ambao wanahisi kuwa wamebambikiwa kesi kufuata utaratibu wa sheria kwa ajili ya kufungua madai yao.

Akimjibu Mbunge wa Kibamba John Mnyika, (chadema) aliyetaka kujua kama endapo wananchi waliobambikiziwa kesi wanaweza kulipwa fidia, Naibu waziri wa Sera, bunge kazi, ajira, Anthony Mavunde alaisema kuwa utaratibu upo wazi.

Naibu waziri alisema kuwa utaratibu wa kimahakama upo wazi kwi mtu anayebambikiwa kesi kwa kufuata sheria zilizopo, na wala serikali haitoi fidia.

Azania Post

Updated: 05.06.2018 14:02
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.