CCM yaeleza siri ya ushindi

CCM yaeleza siri ya ushindi

18 September 2018 Tuesday 12:58
CCM yaeleza siri ya ushindi

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ameitaja siri ya ushindi wa chama hicho kwenye uchaguzi mdogo wa majimbo mawili ya Ukonga na Monduli na kata zote 23 kuwa unatokana na kazi aliyofanywa na inayoendelea kufanywa na Rais John Magufuli.

Polepole amesema hayo leo Septemba 18,2018 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam.

Kauli ya Polepole imekuja kufuatia kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa majimbo ya Monduli na Ukonga ambapo CCM imeshinda majimbo yote.

Amesema mambo yote anayofanya Rais ikiwamo ujenzi  wa barabara, upatikanaji wa maji, upatikanaji wa umeme watu wanaona.

"Tunashukuru tumepokea uaminifu wao kwetu hii umetokana na kuona kila tunachokifanya," amesema Polepole.

Polepole amefafanua kuwa wametoa maelekezo kama chama mawaziri wote, sekta zote waende wakatie kero za wananchi.

Amesema wanatakiwa kuonekana walipo watu wakatatue kero zao.

"Hatutaki watu wakae maofisini kwa sababu siyo sehemu pekee wanapoweza kutatua kero, yote haya watu wanaona," amesema Polepole.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.