CCM yasema haitambui kurejea kwa Lembeli

Yadaiwa hakufuata taratibu kurejea ndani ya chama hicho tawala

CCM yasema haitambui kurejea kwa Lembeli

Yadaiwa hakufuata taratibu kurejea ndani ya chama hicho tawala

15 June 2018 Friday 13:02
CCM yasema haitambui kurejea kwa Lembeli

Chama cha mapinduzi (CCM) wilayani Kahama mkoani Shinyanga kimesema hakina taarifa ya kurejea ndani ya chama hicho kwa James Lembeli kutokana na kushindwa kufuata taratibu na katiba ya chama.

Akizungumza ofisini kwake katibu mwenezi wa CCM wilayani Kahama Joachim Simbila amesema chama kimesikia urejeo wa Lembeli lakini hakuna taarifa rasmi iliyothibitishwa, hivyo alichokifanya ni kuutangazia umma kuwa amehama kutoka Chadema kujiunga na CCM.

Simbila amesema katiba ya chama inasema mwanachama aliyehama chama na kurudi kwa mara ya pili anatakiwa kujaza fomu ambayo itaidhinishwa na tawi la eneo analoishi ambapo wao kama viongozi baada ya kusikia taarifa hizo waliwasiliana na uongozi wa eneo husika lakini hakuna taarifa za James Daud Lembeli kujaza fomu.

Pia Simbila amesema mkutano aliouandaa James Lembeli haukuwa na viongozi wa chama wilaya sambamba na viongozi wa tawi ambapo katika mkutano huo alikuwepo kiongozi wa serikali ya kijiji kitu ambacho kiongozi huyo hana mamlaka ya kumpokea mwanachama mpya kuingia ndani ya chama.

James Lembeli June 13, 2018 alitangaza kuachana na Chadema na kurejea chama cha mapinduzi CCM ambapo alisema ameachana na siasa za majukwaani kwani wazazi wake wote ni waasisi wa TANU ambacho kiliunda CCM hivyo yeye kuwa chama cha upinzani ni kuwakataa wazazi wake.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.