Chadema wajibu mapigo

Chadema wajibu mapigo

04 October 2019 Friday 05:48
Chadema wajibu mapigo

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kinaifanyia kazi barua ya msajili wa vyama vya siasanchini na kwamba kitahakikisha inamfikia ndani ya muda husika uliotajwa wa Oktoba 7, 2019.

Hatua hiyo ni baada ya kukiri kupokea barua ya msajili wa vyama vya siasa  kuhusu kushindwa kufanya uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho ndani ya wakati na kwa nini kisikichukuliwe hatua za kisheria.

Lakini chama hicho kinasema hakijakiuka sheria ya vyama vya siasa wala katiba ya Chadema. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chadema Oktoba 3, 2019

Chadema wamesema katiba ya chama hicho, ibara ya 6.3.3 (a) inatoa mamlaka kwa kamati kusogeza mbele uchaguzi mkuu wa ndani ya chama, na kwamba mamlaka ya kufanya marekebisho hayo yameachwa kwa Kamati Kuu .

Chama hicho kimesema kamati kuu ya chama ilikaa katika kikao chake cha Julai 27 na 28, 2019, na kurekebisha ratiba ya uchaguzi ambapo utakamilika mwezi Disemba kwa ngazi ya taifa na katika hatua zingine

Updated: 04.10.2019 05:56
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.