Chaguzi Afrika zinawezekana bila wizi wa kura? Kwa nini janja ya NASA uchaguzi mkuu Kenya ilishindwa – 1

Chaguzi Afrika zinawezekana bila wizi wa kura? Kwa nini janja ya NASA uchaguzi mkuu Kenya ilishindwa – 1

17 July 2018 Tuesday 09:14
Chaguzi Afrika zinawezekana bila wizi wa kura? Kwa nini janja ya NASA uchaguzi mkuu Kenya ilishindwa – 1

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017 nchini Kenya ulikuwa na mchuano mkali na wa kusisimua sana. Ikiwa Uhuru Kenyatta angeshindwa katika uchaguzi huo, angekuwa ni rais wa kwanza kushindwa kutetea kiti chake akiwa madarakani katika historia ya taifa hilo la Afrika Mashariki.

Ushindi kwa NASA, ulionekana kuwa unawezekana kabisa, kutokana na kujumuika kwa pamoja kwa muungano wa makabila na wagombea kulikofanywa na Raila Odinga ambao hapo awali ilidhaniwa kuwa isingewezekana kabisa.

Mwandishi wa habari JOHN ONYANDO, ambaye alikuwa akifanya kazi na kampeni ya upinzani, anatuletea hadithi ya ndani kabisa ya timu ya Raila kupitia kitabu chake Kenya: The Failed Quest for Electoral Justice.

Katika mfululizo wa kwanza wa sehemu tatu za simulizi yake, anaeleza juu ya machafuko ya ndani na mshangao wa kisiasa ndani ya NASA na jinsi muungano huo wa upinzani nchini humo ulivyopoteza ushahidi wake juu ya wizi wa kura dhidi ya Jubilee kwa ajili ya ombi lake mahakamani. Kila uchaguzi katika maisha ya nchi ni muhimu, lakini uchaguzi wa Agosti 2017 nchini Kenya, ambao alikuja wakati wa machafuko ya kitaifa kayika maeneo mengi nchini humo, ulikuwa, kwa kiasi kikubwa muhimu sana kwa Wakenya kushiriki.

Uchaguzi huo ulikuwa ulichukuliwa kwa dhana mbaya kabisa na vyama vikuu viwili, Jubilee na NASA. Waliingia kwenye uchaguzi huo na mitazamo mibaya kuhusu kile walichokuwa wakitarajia kupata.

Jubilee alijua kwamba Rais Uhuru Kenyatta angeweza kushinda tu muhula wa pili kwa kiwango fulani cha uibaji wa kura, na badala yake walijikuta wakipelekeshwa puta na NASA ambao umaarufu wake ulizidi kupanda kadri siku zilivyokuwa zinakwenda.

NASA kwa upande wake haikuwa imejiandaa kabisa na mpambano dhidi ya kiongozi aliyekuwa madarakani ambaye alikuwa akiungwa mkono na vigogo wakuu wa kitaifa, vyombo vya usalama na jumuiya ya kimataifa.

Hadi kufikia mwezi Mei, Raila Odinga tayari alikuwa na game-plan nzima kichwani juu ya uchaguzi. Niliweza kujua japo kidogo ya alichokuwa akiwaza usiku mmoja baada ya rafiki yake wa muda mrefu na mshauri Salim Lone alipowasili Kenya kuongoza mawasiliano ya kampeni ya NASA.

Lone alikuwa ameniajiriwa kama mhariri wa mtandao wa NASA-NEWS.COM, ambao kampeni ya chama hicho ilipanga kuzindua katika wiki za mwisho ili kuwaelimisha wafuasi wa muungano na kuongeza msingi wa wafuasi wake.

Aliniomba kuhudhuria mkutano wake wa kwanza na Raila nyumbani kwa Waziri Mkuu huyo wa zamani huko Karen jijini Nairobi.

Pia katika mkutano ulioanza saa 2 usiku na kumalizika karibu usiku wa manane alikuwa ni meneja wa kampeni ya Raila, Willis Otieno.

Mapema alasiri hiyo, NASA ilifanya mkutano huko Ongata Rongai, ambapo viongozi wengi wa  viongozi wa Kimasai walikuwa wameelezea kukatishwa tamaa kwa jamii yao na uongozi wa Uhuru na hivyo kujiunga na NASA.

Katika mkutano huo, Raila alizungumza juu ya hali ya kampeni kiujumla, akamgeukia Otieno ili kupata taarifa kidogo, kabla Lone hajanitambulisha.

Nilipokuwa nikizungumza, Bibi Ida Odinga walitembea aliingia ndani ya chumba, na akifuatiwa muda mfupi baadae na Rosemary, ambaye ndiyo kwanza alikuwa amerejea kutoa safari ya matibabu ya mwezi mmoja nchini Afrika Kusini.

Lone alitumia muda mrefu zaidi na wote, na kutuacha sisi watatu kwa muda wa dakika kumi, wakati ambapo Raila alipokuwa akizungumzia zaidi program yake kwa wiki ijayo na Otieno.

Sekretarieti ilikuwa ikikamilisha mikusanyiko ya hadhara magharibi mwa Kenya. Raila alimwuliza Otieno wapi wanapaswa kwenda kwanza kati ya Busia, Kisumu, Migori na Homa Bay.

Kwa mshtuko mkubwa kwa upande wangu, Otieno hakuelewa, akimwacha Raila azungumze kwa muda mrefu zaidi. Nilijiuliza ni kwa jinsi gani alikuwa akiendesha kampeni muhimu kama hii.

Asubuhi iliyofuata, tulifika ofisini kwa kutumia teksi ya Lone majira ya saa 4 asubuhi.

Jimi Wanjigi, ambaye alikuwa amemaliza mkutano, alikuwa akitoka nje, na Lone alimtambulisha kwangu tukiwa bado kwenye parking ya magari. Mara tu baada ya Lone kutamka jina langu la kwanza na Wanjigi alimsaidia kumalizia, kabla ya kusema kwa kunisifu, "Wewe ndio tumekuwa tunasubiri. Tupo nyuma sana kwenye blogu. "

Mpaka siku hiyo, sikuwa nafahamu hata sura ya Wanjigi, lakini nilifurahishwa sana na uchangamfu wake.

Mtazamo wangu wa pili, ukijengeka pale pale, ni juu ya nguvu yake ndani ya NASA. Kabla ya kuingia kwenye gari, Otieno alimkimbilia, akionyesha heshima ambayo kwangu mimi niliona kama heshima ya mwanafunzi kwa mkuu wa shule.

Uwekezaji wa Jubilee katika mitandao ya kijamii ulikuwa unaonekana wazi kutokana na idadi kubwa ya picha za Facebook ambazo zilikuwa zikitamba sana nchini Kenya wakati wa uchaguzi.

Chama kilikuwa na tovuti tano za kampeni. Ilikuwa na ushawishi zaidi kwenye Facebook.

Itaendelea...

Imetafsiriwa kutoka mtandao wa www.standardmedia.com

Updated: 17.07.2018 09:32
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.