CUF yawashukia wabunge wanaotetea hadhi ya Maalim Seif bungeni

Kumekuwa na mgogoro wa uongozi ndani ya chama cha upinzani cha CUF kwa muda mrefu sasa

CUF yawashukia wabunge wanaotetea hadhi ya Maalim Seif bungeni

Kumekuwa na mgogoro wa uongozi ndani ya chama cha upinzani cha CUF kwa muda mrefu sasa

06 June 2018 Wednesday 15:14
CUF yawashukia wabunge wanaotetea hadhi ya Maalim Seif bungeni

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Habari, uenezi na mahusiano ya Umma ya chama cha Wananchi CUF, Abdul Kambaya, amesema kuwa wabunge wengi wamekuwa wakitetea na kulinda hadhi ya Katibu Mkuu wa chama hicho Seif Shariff Hamad na kuacha majukumu yao.

Chama hicho kimedai kusikitishwa na hatua ya wabunge hao waliochaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwakilisha matatizo yao badala yake baadhi ya yao wameacha jukumu hilo na kujipa jukumu jipya la kulinda hadhi ya Maalim Seif.

Mkurugenzi huyo amesema ni takribani miaka miwili sasa wabunge hao kila wanaposimama hujenga hoja za kutetea Ukatibu Mkuu wa Maalim Seif badala ya kujenga zitakazotatua changamoto zilizopo kwenye majimbo yao kwa kushirikiana na serikali kupitia wizara husika.

“CUF imesikitishwa na inawaomba radhi Watanzania kutokana na vitendo vya baadhi ya wabunge hao. Ni jambo la kufedhehesha na kutia aibu sana kupokea posho na mshahara kutoka kwa walipa kodi wa Tanzania kisha unatumia miaka miwili ndani ya vikao vya Bunge kutetea hadhi ya mtu badala ya kujenga hoja zenye manufaa na walipa kodi wa Tanzania.

“Suala la ruzuku ya CUF na matumizi yake ni jambo la kisheria pale ambapo Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) atabaini upotevu wa fedha hizo atatoa taarifa kwa umma, kwa hiyo kujificha kwenye hoja hiyo kwa lengo la kumfanya Maalim Seif aishi kisiasa si tu ni matumizi mabaya ya posho na mishahara  inayotolewa na Bunge lakini pia ni kutotambua wajibu wao kwa wapiga kura wao waliowachagua.”

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.