banner58

David Kafulila amshukia Freeman Mbowe

Amtaja Lowassa kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi zaidi

David Kafulila amshukia Freeman Mbowe

Amtaja Lowassa kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi zaidi

04 June 2018 Monday 12:14
David Kafulila amshukia Freeman Mbowe

Na Amini Nyaungo

Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila amesema Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kina Mwenyekiti wa kudumu asiyebadilika.

Akiongea hayo kupitia Times FM amesema chama hicho kinatakiwa kujifakari na kutoa Demokrasia ya kweli ya kuwapa nafasi wanachama kugombea nafasi hiyo kama vilivyo kwa vyama vingine.

Alisema uamuzi wake wa kujivua uanachama wa Chadema ilikuwa na lengo la kutoa changamoto ndani ya chama hicho.

"Demokrasia inatakiwa uwe nayo wewe kwanza, kwa sababu kama kweli unapigania demokrasia tangu serikali zilizopita hadi leo bado mwenyekiti wewe, nani ataamini kama Demokrasia ipo,"amesema.

Maneno yake yanaonekana kumlenga Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye ndiye amekaa muda mrefu akiwa kama mwenyekiti wa chama hicho.

Aidha katika hatua nyingine Kafulila amesema hakuna chama kinachoweza kukidhi mahitaji yote ya wananchi, hivyo kama taifa imara inahitajika katiba nzuri.

Pia ameweza kuthibitisha kuwa Lowassa ndiye mwanasiasa aliyekuwa na ushawishi mkubwa mwakani 2015. 

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.