Dk Bana ataja mtihani wa kwanza kwa Katibu Mkuu mpya wa CCM

Alipoulizwa kama alitarajia jina la Bashiru kuwa Mtendaji mkuu wa chama, Dk Bana alisema kuwa siyo mara ya kwanza kutajwa lakini kwa zamu hii haikuwa rahisi.

Dk Bana ataja mtihani wa kwanza kwa Katibu Mkuu mpya wa CCM

Alipoulizwa kama alitarajia jina la Bashiru kuwa Mtendaji mkuu wa chama, Dk Bana alisema kuwa siyo mara ya kwanza kutajwa lakini kwa zamu hii haikuwa rahisi.

30 May 2018 Wednesday 09:04
Dk Bana ataja mtihani wa kwanza kwa Katibu Mkuu mpya wa CCM

Na Mwandishi Wetu

MHADHIRI mwandamizi wa masuala ya sayansi ya jamii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Benson Bana, amesema mtihani wa kwanza kwa Katibu Mkuu mpya wa CCM , Dk Bashiru Ally aliyeteuliewa jana ni kusimamia mapendekezo ya Tume aliyokuwa ainaiongoza Akizungumza na Azania Post leo asubuhi Mei 30, 2018 , Dk Bana alisema kuwa Katibu Mkuu huyo mpya awali aliteuliwa na Mwenyekiti wa CCM Dk John Magufuli kuhakiki mali zote za chama hicho kikongwe hapa nchini.

Alisema kuwa Dk Bashiru alifanya kazi nzuri sana kwa kuisimamia vizuri tume aliyokuwa anaiongoza na sasa anatakiwa kusimamia utelekezaji wa mapendekezo yake.

Dk Bana alisema kuwa endapo Katibu Mkuu huyo atayafanyia kazi mapendekezo ya Tume hiyo itakuwa ni ushindi kwa chama , na kielelezo cha utumishi uliotukuka.

Alipoulizwa kama alitarajia jina la Bashiru kuwa Mtendaji mkuu wa chama, Dk Bana alisema kuwa siyo mara ya kwanza kutajwa lakini kwa zamu hii haikuwa rahisi.Alifafanua kuwa nafasi hiyo imempata mwenyewe kwani ni mwanafunzi wake ambaye anamjua ni mzalendo na anakifahamu vizuri chama tangu kuasisiwa kwake.

“Bashiru ni mwaminifu na misimamo yake kuhusu kutetea watu wanyonge inarandana kwa ukaribu na ya mwenyekiti Magufuli”, alisema

Alidokeza kuwa Bashiru hakuwa ni mwanasiasa wa jukwaani . lakini ni mtu mwepesi sana wa kujifunza na kuwa atafanya hivyo kupitia kwa watangulizi wake

Changamoto nyingine ambayo Katibu Mkuu huyo mpya anatarajiwa kupambana nayo ni kukiimarisha chama kuanzia ngazi ya tawi, kata, wilaya hata baadhi ya mikoa, alisema

Kwa mujibu wa Dk Bana kwa sasa chama kimedorora kwani kipo mbali na wananchi na kazi yake kubwa itakuwa ni kujibu matatizo ya wanyonge kulingana na ilani.

Alisema kuwa Dk Bashiru anatakiwa kuimarisha jumuiya za chama tawala ili watu wakielewe zaidi .

Kuhusu Katibu Mkuu anayemrithi Abdulrahaman Kinana, alisema kuwa alikihudumia chama vizuri kwani kuna wakati kilipoteza mvuto.

Akikabidhi ripoti ya tume yake kwa Rais Magufuli wiki iliyopita, Dk Bashiru alisema kuwa uhakiki wa miezi mitano umefanyika kwa kutembelea maeneo yenye mali za chama, kuwahoji watu mbalimbali wakiwemo viongozi waliohusishwa na mali zilizokuwa zikihakikiwa, upitiaji wa nyaraka na kufuatilia uhalisia katika ofisi za mamlaka husika, kufanya uchambuzi wa taarifa na kutoa mapendekezo.

Ameongeza kuwa uhakiki huo umefanyika katika mali za chama zilizo chini ya baraza kuu, jumuiya za chama na kampuni za chama.

Katika tume imebaini uwepo wa upotevu mkubwa wa mali za chama uliosababishwa na mikataba mibaya, ubadhilifu, wizi, usimamizi mbaya wa mali, utapeli na ukosefu wa maadili katika uendeshaji wa miradi ya chama.

Kwa upande wake Rais Magufuli aliwaaagiza wajumbe wa sekretarieti ya CCM waliohudhuria wakati wa uwasilishwaji wa ripoti hiyo kuanza kufanyia kazi baadhi ya mambo yaliyo ndani ya uwezo wao na kwamba masuala mengine yataamuliwa na vikao vikuu vya chama.

Azania Post

Updated: 30.05.2018 09:30
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.