Dk Mzindakaya awashangaa wanaomwita JPM dikteta

Dk Mzindakaya awashangaa wanaomwita JPM dikteta

11 September 2018 Tuesday 13:07
Dk Mzindakaya awashangaa wanaomwita JPM dikteta

Sumbawanga, Tanzania

Mwanasiasa Mkongwe, Dk Chrisant Mzindakaya ameeleza kukerwa na kauli za baadhi ya wanasiasa nchini wanaodai Rais John Magufuli ni kiongozi anayetawala kwa mabavu (dikteta).

Akizungumza na Mwananchi leo Septemba 11, Dk Mzindakaya amsema wanasiasa wa aina hiyo wamefilisika kisiasa na walizoea utawala wa kubembelezana hivyo ni lazima wabadilike na kuendana na kasi ya utawala wa kiongozi wa sasa.

"Kuna watu waliwahi kudiriki kuandika katika mitandao ya kijamii wakidai umefika wakati tunataka Rais mkali, mwenye kufanya maamuzi.......sasa amekuja Magufuli ambaye mimi naamini anasimamia maamuzi na misingi ya haki na sheria za nchi, baadhi ya watu wanadai ni dikteta, " alisema Dk Mzindakaya.

Amesema tatizo la Watanzania si wepesi kukubali mabadiliko ya kiutawala kwani aina ya utawala wa Rais Magufuli unakwenda kwa kasi na msukumo wa nguvu kitu ambacho wengi walikuwa hawajazoea hivyo wanapaswa kubadilika na kuendana na kasi hiyo badala ya kulalama pasipo na tija.

Dk Mzindakaya alitolea mfano yeye akiwa mkuu wa mkoa wa Morogoro enzi za Rais wa kwanza wa nchi hii, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kutuhumiwa akiongoza mkoa huo kwa misingi ya mabavu kitu ambacho si kweli ila alitaka watu wawajibike kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.