Halima Mdee afanyiwa upasuaji, alazwa

Halima Mdee afanyiwa upasuaji, alazwa

08 June 2019 Saturday 17:03
Halima Mdee afanyiwa upasuaji, alazwa

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
MJUMBE wa kamati kuu ya Chadema, Halima Mdee amefanyiwa upasuaji uliochokuwa takribani saa nne na nusu.

Upasuaji huo umefanyika  Juni 7,2019 katika hospitali ya Aga Khan na anaendelea vizuri na matibabu hospitalini hapo.


Taarifa  iliyosainiwa na mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene inaeleza kuwa Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe, alilazwa hospitalini hapo tangu Alhamisi Juni 6, 2019.

Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) Taifa na alilazimika kufanyiwa upasuaji baada ya kushauriwa na madaktari wake kwa ajili ya kutibu ugonjwa uliokuwa unamsumbua.

"Baada ya upasuaji huo uliochukua takriban muda wa saa 4.30, Mhe. Mdee bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari, akiendelea kuimarika na kupata nguvu, ambapo madaktari wameshauri apate muda wa kupumzika kabla hajaruhusiwa kutoka hospitalini hapo"

Updated: 08.06.2019 17:11
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.