banner68
banner58

Halmashauri Monduli yarejea CCM

Halmashauri Monduli yarejea CCM

11 August 2018 Saturday 16:33
Halmashauri Monduli yarejea CCM

Unaweza kusema halmashauri ya Monduli Mkoa wa Arusha ambayo ilikuwa inaongozwa na Chadema imerejea CCM baada ya madiwani 10 wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini kujiuzulu na kujiunga na chama tawala.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumamosi Agosti 11, 2018 mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Steven Ulaya amesema baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Chadema walipata madiwani 18, wakiwemo wa viti maalum watano huku CCM ikipata madiwani tisa, wawili wakiwa wa viti maalum.

“Tayari CCM imeshinda kata sita katika chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika, bado kuna uchaguzi katika kata mbili, ikiwemo ya Monduli baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo kujiuzulu. Pia aliyekuwa mbunge (wa Chadema Monduli-Julius Kalanga) amejiuzulu,” amesema.

Amesema kwa sasa Chadema imebaki na madiwani tisa, wakiwemo watano wa viti maalum.

Akizungumza wimbi la madiwani kujiuzulu, Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Aman Golungwa amesema kinachofanywa na wanaohama ni mchezo mchafu, kusisitiza kuwa chama hicho hakiwezi kufa, “waache waondoke ila wananchi wanajua kinachoendelea.”

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema wanaotaka kuondoka katika chama hicho wasijifiche, kuwataka watoe taarifa na wataagwa.

“Tunasema waache waondoke kwa ajili ya shida zao binafsi sisi tutabaki na kamwe wasidhani Chadema itakufa,” amesema.

Mpaka sasa madiwani 31 wa Chadema mkoa wa Arusha wamejiuzulu na kujiunga na CCM.

Mwananchi

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.