banner68
banner58

Hatujazuia shughuli za siasa nchini - serikali

Hatujazuia shughuli za siasa nchini - serikali

07 May 2018 Monday 11:52
Hatujazuia shughuli za siasa nchini - serikali

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imekanusha kuwa imezuia harakati za kisiasa kufanyika nchini Tanzania, lakini imesema kuna utaratibu maalum wa kuzifanya shughuli hizo.

Hayo yameelezwa Bungeni leo Jumatatu Mei 7 na Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo, Joseph Selasini (Chadema).

Mbunge huyo alitaka serikali kueleza sababu za polisi kuzuia hata vikao vya ndani vya vyama vya siasa na kuitaka kuleta sheria ya mabadiliko.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Mavunde, alisema kuwa si kweli kuwa serikali imezuia harakati za kisiasa lakini kuna utaratibu maalum umewekwa ili kufanya kazi hiyo.

Alisema kuwa kuna sheria inayoruhusu jeshi la polisi kuhakikisha kuwa vyama hivyo vinafanya kazi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Hata hivyo alibainisha kuwa kuna mafanikio na changamoto nyingi ambazo Tanzania imeziona tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Alitaja baadhi ya faida kwa ni kupanuka kwa demokrasia ambapo hadi sasa kuna vyama vya siasa 19 vilivyosajiliwa, uchaguzi na kuongezeka kwa uwazi na utendaji wa serikali

Changamoto ni pamoja na kuongezeka kwa gharama zinazotokana na uchaguzi, makundi ndani ya vyama na kuchochea vurugu wakati wa kampeni na kushuka kwa uzalendo kutokana na mtizamo hasi dhidi ya serikali iliyopo madarakani.

Kuhusu Msajili wa vyama vya siasa, kuingilia kati shughuli za siasa, alisema kuwa sheria namba 7 ya mwaka 2009 inampa madaraka kufanya hivyo.

Alisema kuwa yeye ni kama mlezi wa vyama vyote na kunapotokea chochote kinyume na maadili lazima aingilie kati.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Jumbe 2018-05-07 12:45:12

Yangu macho na maskio huyu waziri sijui anamuogopea nani au anamuofia nani akisema kweli

Avatar
Jumbe 2018-05-07 12:46:05

Yangu macho na maskio huyu waziri sijui anamuogopea nani au anamuofia nani akisema kweli