Jordan yakumbwa na maandamano bila kikomo licha ya Waziri Mkuu kuachia ngazi

Taarifa zinasema kuwa kujiuzulu kwa Mulki juzi kumekubaliwa na Mfalme Abdullah wa taifa hilo la mashariki ya Kati

Jordan yakumbwa na maandamano bila kikomo licha ya Waziri Mkuu kuachia ngazi

Taarifa zinasema kuwa kujiuzulu kwa Mulki juzi kumekubaliwa na Mfalme Abdullah wa taifa hilo la mashariki ya Kati

05 June 2018 Tuesday 18:13
Jordan yakumbwa na maandamano bila kikomo licha ya Waziri Mkuu kuachia ngazi

Na Mwandishi Wetu

WANANCHI wa Jordan wameendelea kuandamana licha ya kujizulu kwa waziri mkuu wa taifa hilo, Hani Mulki.

Taarifa zinasema kuwa kujiuzulu kwa Mulki juzi kumekubaliwa na Mfalme Abdullah wa taifa hilo la mashariki ya Kati.

Mulki aliitwa na mfalme huyo kufuatia siku tano za maandamano dhidi ya hatua za kubana matumizi zilizopangwa kutekelezwa na serikali ya taifa hilo la kifalme.

Watu 60 wamekamatwa kwa kuandamana na kubeba visu wakati wa maandamano hayo.

Kulingana na duru za serikali, Omar al-Razza, mchumi wa zamani wa Benki ya Dunia na waziri wa sasa wa elimu, ametakiwa na mfalme kuunda serikali mpya.

Mkuu wa muungano wa wafanyakazi amesema maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumatano yataendelea mpaka msuada wa sheria ya kodi ya mapato ufutwe.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.