Kalanga ashinda Monduli, aahidi makubwa

Kalanga ashinda Monduli, aahidi makubwa

17 September 2018 Monday 12:12
Kalanga ashinda Monduli, aahidi makubwa

MBUNGE mteule katika jimbo la Monduli aliyeshinda kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika jana tarehe 16 Septemba 2018 kwa kura asilimia 95, Julius Kalanga ameahidi kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zilizomo kwenye jimbo hilo, hasa migogoro ya ardhi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 20.

Kalanga ametoa ahadi hiyo baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo na Msimamizi wa Uchaguzi Monduli, Steven Ulaya usiku wa kuamkia leo tarehe 17 Septemba 2018.

“Napenda kuchukua fursa hii kukishukuru Chama cha Mapinduzi CCM na mwenyekiti wake na wanachama pamoja na wananchi wa jimbo hili tulioshirikiana nao katika jambo hili. Nashukuru tulifanya kampeni za kistaarabu jimbo letu limebaki na amani,” amesema na kuongeza Kalanga.

“Yako mambo ya msingi tuliyokubaliana na wananchi nilioingia nao mkataba, wananchi waliniamini walinipa kura yao. Yako mambo ya msingi ya kufanya, jambo la kwanza ni maji, maeneo mengi ni kame, pili nitrashirikiana na serikali ili kutafutia ufumbuzi, kuondoa migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda wa miaka 20 kutafutia ikiwemo kubainisha mipaka.”

Katika uchaguzi huo, Kalanga alichuana na Yonas Laizer wa Chadema aliyepata kura 3,187 ,Wilfred Mlay wa ACT Wazalendo  (144), Feruz Juma wa NRA (45), Simon Ngilisho wa Demokrasia Makini (35), Omary Juma wa DP (34), mgombea wa ADA-Tadea, Francis Ringo (21) na Elizabeth Salewa wa chama cha Wakulima aliyepata kura 16.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.