Katibu Mkuu CCM atema cheche

Katibu Mkuu CCM atema cheche

13 June 2018 Wednesday 17:59
Katibu Mkuu CCM atema cheche

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema atawafukuza uanachama watendaji wote watakaoonekana wanabeba mikoba ya wagombea na kushabikia makundi ya siasa ndani ya chama hicho.

Dk Bashiru ameyasema hayo leo Juni 13 akiwa katika makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma wakati akizungumza na wanachama pamoja na watumishi wa chama hicho mkoani hapa.

Amesema ni marufuku watendaji wa chama hicho kuwa na makundi ya siasa ndani kwani hali hiyo ikitokea chama hakiwezi kuendelea mbele.

“Ni marufuku mtendaji wa chama kumshangilia mgombea wa kisiasa, kwani hiyo inapelekea kuwa na makundi, sasa tujiulize kila mtendaji akiwa na mgombea wake chama kitakalika?

“Hivyo nitawafukuza watendaji wote ambao wataonekana wanabeba mikoba wa wagombea, waacheni wanachama wa kawaida wafanye hivyo ila si ninyi watendaji ambao mnalipwa hela za wananchama,” amesema.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Lanwell Mungu 2018-06-13 18:37:32

Nikweli mkuu