Katibu mwenezi Chadema auwawa kwa kupigwa risasi

Katibu mwenezi Chadema auwawa kwa kupigwa risasi

13 June 2019 Thursday 17:01
Katibu mwenezi Chadema auwawa kwa kupigwa risasi

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
CHAMA cha Chadema kimesema kinafuatilia kwa undani kuhusu kifo chenye utata cha Katibu Mwenezi wa chama hicho jimbo la Malinyi mkoani Morogoro, Lucas Lihambalimu.

Taarifa ya chama hicho inaeleza kuwa kiongozi huyo alivamiwa nyumbani kwake, kupigwa risasi na kufariki papo hapo majira ya saa nane usiku.

"Eneo hilo la bonde la kilombero pia aliuwawa diwani wa Chadema, Lwena kwa kukatwa mapanga'' inaeleza taarifa hiyo

Taarifa za awali zimedai kuwa watu wenye silaha walifika nyumbani kwa marehemu wakagonga wakimtaka atoke kuwa wana shida naye.

Akiwa anatafuta upenyo wa kuchungulia kuwajua ni akina nani, walimfyatulia risasi kichwani na kumuuwa papo hapo.

Updated: 14.06.2019 08:28
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.