Kesi kupinga sheria mpya vyama vya siasa yaahirishwa kwa muda

Kesi kupinga sheria mpya vyama vya siasa yaahirishwa kwa muda

19 June 2019 Wednesday 12:26
Kesi kupinga sheria mpya vyama vya siasa yaahirishwa kwa muda
Na mwandishi wetu, Arusha
JOPO la majaji watano wa mahakama ya Afrika Mashariki(EACJ) limeahirisha kwa muda usikilizaji wa kesi ya kupinga sheria mpya ya vyama vya siasa ili kufanya majadiliano ya kama waendelee kusikiliza kesi upande wa walalamikaji ama kuishirikisha serikali ya Tanzania.
Hata hivyo baadae hii leo Juni 9, 2019 jopo hilo  uenda likatoa uamuzi huo.
Jopo hilo limesikia kwa mara ya kwanza maombi madogo na 2/2019 yanayotokana na shauri na 3/2019 lililofunguliwa hapo kupinga sheria ya vyama vya siasa na 1 ya mwaka 2019.

Washtaki wanaiomba  mahakama ya EACJ isimamishe matumizi ya sheria hiyo hadi kesi ya msingi itakapoamriwa.

Walalamikaji katika shauri hilo ni muungano wa vyama nane vya kisiasa wakiwakilishwa na Freeman Mbowe, Maalim Seif Sharif Hamad, Zitto Kabwe na Salum Mwalimu kupitia maombi yao wanaiomba mahakama hiyo izuie sheria hiyo kwa muda hadi shauri namba 3/2019 litakapoamriwa, kwa sababu utekelezaji wake unaendelea kuwaathiri.

Majaji waliosikiliza kesi hiyo ni  Jaji Fakihi Jundu(Tanzania), Charles Nyachai(Kenya), Monica Mugenyi(Uganda), Faustine Ntezilyago(Rwanda) na Charles Nyawelo(Sudani Kusini)

Walalamikaji wanawakilishwa na mawakili Fatma Karume, Mpale Mpoki, Jebra  Kambole na John Mallya

Updated: 20.06.2019 14:16
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.