Kesi ya Zitto, shahidi atoa la moyoni

Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, anadaiwa kutenda makosa hayo, Oktoba 28,2018 katika mkutano na waandishi wa habari

Kesi ya Zitto, shahidi atoa la moyoni

Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, anadaiwa kutenda makosa hayo, Oktoba 28,2018 katika mkutano na waandishi wa habari

16 May 2019 Thursday 14:45
Kesi ya Zitto, shahidi atoa la moyoni

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

SHAHIDI wa pili katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe hii leo Mei 16, 2019 ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi alivyolichukia jeshi la polisi baada ya kusikia kwenye video iliyopo kwenye mtandao wa kijamii wa you tube.

Shahidi huyo Mashaka Juma ambaye ni msanii wa filamu amedai video hiyo ilikuwa ikimuonyesha Zitto Kabwe akielezea polisi walivyoenda kuwachukua watu hospitali na kwenda kuwaua.

Katika kesi hiyo , Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, anadaiwa kutenda makosa hayo, Oktoba 28,2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Akiongozwa na Wakili wa serikali Mkuu Tumaini Kweka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi leo Mei 16,2019 Shahidi huyo amedai Oktoba 29,2018 akiwa eneo la Kimara Korogwe na wenzake wanacheza mchezo wa drafti wakati wakiendelea na mchezo huo alikuja mwenzao ambaye anaitwa Frenky Zongo.

Amedai alipofika alituuliza sisi kama tumepata habari yeyote lakini tulimweleza hatujui ndipo akatuambia Zitto ndie habari ya mjini na kututolea simu yake kisha akatufungulia na tukaangalia habari kwenye yuotube.

Shahidi huyo ameeleza wakati wanaangalia walimwona Zitto akililaumu jeshi la polisi kwa mambo mbalimbali ambayo wameyafanya wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma.

Amedai, katika video hiyo inamuonyesha Zitto akieleza jinsi jeshi la polisi likiwanyanyasa wananchi,kuteka watu akiwemo aliemtaja kwa jina la Mo wa Simba na polisi walivyoenda hospitali kuwateka watu waliokuwa wakitibiwa na kwenda kuwaua.

Aliendelea kueleza, katika video hiyo inamuonyesha Zitto akielezea jinsi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini alivyoshindwa kuwadhibiti askari wake .

Shahidi huyo amesema, kwa kuwa Zitto anamfahamu tangu akiwa Chadema na akiwa mfuasi wake hadi leo akiwa ACT Wazaledo binafsi alimuamini kutokana na taarifa hiyo, aliona jeshi la polisi halina thamani kama wameshindwa kulinda raia na mali zake ndipo alipolichukia hadi leo jeshi hilo.

Kesi hiyo itaendelea kesho kwa upande wa mashtaka kuendelea kuleta mashahidi

Updated: 16.05.2019 19:17
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.