Kesi ya Zitto yaendelea kupigwa 'danadana'

Kesi ya Zitto yaendelea kupigwa 'danadana'

18 June 2019 Tuesday 12:53
Kesi ya Zitto yaendelea kupigwa 'danadana'

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam  imeshindwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa sababu upande wa mashitaka umekosa kibali cha kuita mashahidi kutoka mkoani Kigoma.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga  amesema  hayo leo Juni 18, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja  kuendelea kusikilizwa.

Kesi hiyo leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, wakili Katuga amedai, shauri hilo lilipangwa kusikilizwa na walishaanza utaratibu wa kupata mashahidi kutokea mkoani Kigoma lakini wamekosa kibali kutoka kwa Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 16 na 17, 2019.

Katika kesi ya msingi, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anadaiwa kutenda makosa hayo, Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Updated: 18.06.2019 13:41
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.